ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 9, 2012

MBUNGE CHADEMA ASHINDA KESI YA UCHAGUZI MZ.

Wakili T. Lisu (kulia) ndiye aliyesimamia kidete kesi hiyo iliyompa ushindi mteja wake mbunge Highness Kiwia.
Mahakama kuu ya kanda ya Mwanza imemwachilia huru mbunge wa Ilemela Highness Kiwia kutokana na kesi ya madai namba 12 ya mwaka 2010, iliyo funguliwa na walalamikaji watatu ambao ni Lupilya, Nsubuga pamoja na Madenge, ambapo waliiomba mahakama Kuu Kanda ya Mwanza itengue ushindi wa Mbunge wa huyo kupitia CHADEMA, kwa madai kwamba mbunge huyo hakushinda kihalali kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Jaji Mjema alihitimisha kusoma hukumu hiyo kwa kusema kwamba: "Kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa na walalamikaji pamoja na upande na maelezo ya wa wadaiwa, mahakama hii inatupilia mbali mashtaka haya, na walalamikaji wanapaswa kulipa gharama zote za kesi hii".

"Kwa kweli huu ni ushindi wa kihistoria kwa nchi hii ya Tanzania. Lakini naamini kesi ni gharama na nitawafungulia kesi hawa watu ili walipe gharama zote nilizotumia. Nitakaa na mwanasheria wangu Tundu Lisu tuone gharama kiasi gani tumetumia", alisema Mbunge Kiwia huku akishangiliwa na mamia ya wafuasi wake.

Jaji Gadi Mjema akitoa hukumu hiyo leo amesema ushahidi uliotolewa na wakazi hao hautoshelezi na hivyo mahakama imemuachia huru mbunge huyo dhidi ya kesi iliyokuwa ikimkabili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.