ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 30, 2011

TAQWA SEC MABINGWA AIRTEL RISING STAR KITUO CHA MWANZA

Kipa wa timu mabingwa Taqwa Sekondari Damian Paul(16) na makeke yake langoni.

Fainali ya Airtel Rising Star imefanyika leo jioni kwenye kituo cha mwanza viwanja vya Buswelu Sekondari ambapo leo kulikuwa na michezo miwili, mchezo wa kwanza umeshuhudia Mwanza Sekondari wakiibuka nafasi ya tatu mara baada ya ushindi wa bao 1 dhidi ya Buswelu sekondari goli likipatikana kwa njia ya penati (pichani) mfungaji akiwa ni Selemani Ibrahimu aliyefanikiwa kumhadaa kwa ufundi kipa wa timu pinzani.

Mabingwa Taqwa Sekondari.

Aka Chicharito mchezaji wa Taqwa aliyekuwa mwiba kwa Nsumba.

Nsumba Sekondari.

Mchezo wa pili wa fainali ulikuwa ni kati ya Nsumba Sekondari na Taqwa kipute kilichoanza kwa kasi ya ajabu na ushindani mkubwa lakini hadi dakika za kawaida za mchezo zinamalizika ngoma droo 0-0 ndipo ikaamuliwa njia ya matuta iliipa ushindi Taqwa kwa penati 4-3, penati zilipigwa nane, nane.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.