Pamoja na kukabidhiwa kombe la ubingwa pia timu hiyo imejizolea kitita cha shilingi 500,000/= seti moja ya jezi na mpira mmoja..
Kwaniaba ya timu yake kapteni wa Ngano fc toka kata ya Ngudu akipokea zawadi ya mshindi wa pili ambayo ni Jezi seti moja na kitita cha shilingi 300,000/= toka kwa mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Kwimba bw. Christopher Kangoye, kutoka kushoto ni katibu wa CCM wilaya ya Kwimba Petronila Kichele, Mkuu wa wilaya, katibu Mwenezi Ledenta Majigwa na Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilayani Kwimba (KWIDEFA) Michael Matola.
Tuzo rahaaaa.... Hapa ni kocha wa timu ya Mwahobha Fc akichekelea tuzo iliyozawadiwa timu yake kama Timu yenye nidhamu mashindanoni.
Washindi wa tatu ni Polisi Ngudu ambao walipata zawadi ya shilingi 150,000/= Lengo la kuanzishwa kwa Mashindano haya ni kuibua na kukuza vipaji jimbo la Kwimba, Kukutanisha wananchi katika suala zima la Umoja na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhusu ukuzaji wa Michezo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.