Uamuzi huo umetokana na timu ya Taifa (Taifa Stars) kuwa na mechi ya kirafiki katika kalenda ya FIFA (FIFA dates) ugenini itakayochezwa Agosti 10 mwaka huu dhidi ya Palestina. Stars itarejea nchini Agosti 11 mwaka huu baada ya mechi hiyo.
Wachezaji wengi wanaounda kikosi cha Taifa Stars kwa sasa wanatoka katika klabu hizo mbili. Awali Stars ilikuwa icheze mechi nyingine Agosti 13 mwaka huu jijini Amaan wakati aikitokea Palestina. Kocha Mkuu wa Stars, Jan Poulsen ameifuta mechi hiyo kwa vile Jordan haitakuwa na wachezaji wake wa kulipwa kutokana na kuwa nje ya kalenda ya FIFA.
FAINALI LIGI YA TAIFA
Fainali ya Ligi ya Taifa itakayoshirikisha timu 12 zitakazo gawanywa katika makundi matatu ya timu nne nne itafanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kuanzia Agosti 6 mwaka huu.
Awali ligi hiyo ilianza katika vituo vinne ambapo timu tatu za juu ndizo zilizo pata tiketi ya kucheza fainali. Kituo cha Pwani kimetoa timu za Cosmopolitan (Ilala), Sifapolitan (Temeke) na Mgambo Shooting (Tanga) wakati Samaria (Singida), Majengo SC (Dodoma) na Morani (Arusha) zimefuzu kutoka kituo cha Singida.
Police Central (Ilala), Small Kids (Rukwa) na JKT Mlale (Ruvuma) zimefuzu kutoka kituo cha Rukwa wakati kituo cha Kigoma kimetoa timu za Kasulu United (Kigoma), Geita Veterans (Mwanza) na Rumanyika SC (Kagera).
Timu zinatakiwa kuwasili Tanga siku mbili kabla ya fainali kuanza ambapo mshindi wa kwanza katika kila kundi pamoja na washindwa bora (best losers) wawili watapanda hadi daraja la kwanza.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.