Katika mchezo huo wa pili Taqwa waliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Buswelu (pichani).
"Mcheze mpira mzuri, uliojaa ushindani pamoja na ufundi mkiwa na nidhamu ndani yake, kumbukeni kuwa siyo wote mtaenda ngazi ya taifa bali ni vijana sita hivyo itumieni vyema nafasi hii kuiwakilisha Mwanza na sehemu yake ya ajira kwa zama zijazo. Kila mmoja acheze akiweka nadhiri moyoni mwake kuwa MIMI LAZIMA NIWE KATI YA WALE SITA" @Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro.
Kwenye mchezo wa awali leo nayo Nsumba Sekondari imeibamiza timu yenye majigambo mengi vijana wa mjini Mwanza Sekondari 1-0
Taqwa Sekondari ( red) wakipeleka mashambulizi langoni mwa Buswelu Sekondari hekaheka zilizozaa bao la ushindi.
Kwa mujibu wa mratibu wa mashindano hayo mkoa wa Mwanza Job Mushumba amesema kuwa michezo ya ligi hiyo katika hatua inayofuata itachezwa kwa njia ya mtoano yaani Fist looser kucheza na Second looser kupata mshindi wa tatu na First winner kucheza na Second winner kumpata bingwa wa kituo cha Mwanza,
Michezo yote hiyo inataraji kuchezwa jumamosi ya wiki hii kiwanja nitakwambia papahapa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.