KARAGWE
Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na VVU Katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera yameshuka kutoka asilimia 2.3 mwaka 2022 mpaka kufikia asilimia 1.3 kwa waliojitokeza kupima January -November mwaka huu
Akisoma risala mbele ya Mgeni Rasmi ,Afisa mtendaji wa Kata ya Bugene Happyness Kanyoro ,katika maadhimisho ya kumbukizi ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Bugene amesema hali ya maambukizi mapya katika wilaya yanapungua ukilinganisha na miaka iliopita
Akitaja takwimu za miaka iliopita amesema zinapungua kutokana na mwitikio wa watu kujitokeza kupima afya zao na kufuata ushauri wa taalama na kusema kuwa kwa mwaka 2020 hali ya maambukizi ilikuwa asilimia 5,mwaka 2021 3.2,mwaka 2022 asilimia2.3,
Wakitoa ushuhuda baadhi ya watu ambao wamepata maambuzi ya virusi vya Ukimwi kwa zaidi ya mika 20 ,wamewaondoa hofu baadhi ya watu wanaogopa kupima na waliogundulika na kuwahimiza kupima jambo litalowasaidia kujitambua na kujikubali
Naye Mgeni Rasmi,Mwk wa kamati ya Kudhibiti Ukimwi Wilaya ya Karagwe Dauson Byamanyirwoi ambae pia ni Diwani wa kata ya Rugera kupitia maadhimisho hayo amemuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii kushirikina kwa kutoa elimu na kuhakikisha wanatoa huduma ya tohara vijijini ili kusaidia kupungua maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na VVU.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yameambatana na kauli mbiu isemayo Jamii iongoze kutokomeza Ukimwi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.