Waandamanaji nchini Bukina Faso wameteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, kupinga hatua ya kuongeza muhula wa Rais Blaise Compaore ambaye ametawala nchi kwa miaka 27.
Runinga ya itaifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.
Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.
Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.
Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.
Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.
Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.
Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987. Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.