Tangu Julai 2010, kituo cha uzalishaji Bora na Hifadhi ya Mazingira Tanzania (CPCT) kikishirikiana na vituo mwenza vya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki kimekuwa kikihamasisha utekelezaji wa mbinu na teknolojia zenye kuleta ufanisi katika matumizi ya rasilimali na kupunguza uchafuzi wa mazingira katika viwanda na shughuli za kibiashara ndani ya bonde la Ziwa Victoria chini ya mwavuli wa Mradi wa Usimamizi wa Mazingira ya Ziwa Victoria - Awamu ya pili (LVEMP-II).
LVEMP-II ni mradi unaotekelezwa na nchi tano zinazozunguka bonde la Ziwa Victoria, hususan Burundi, kenya, Rwanda, Uganda na Tanzania, tangu September 2009 hadi Juni 2014.
Madhumuni makuu ya mradi kijenzi (Project sub-component) wa uzalishaji bora na upunguzaji uchafuzi wa mazingira (cleaner production) chini ya LVEMP-II ni kupunguza msongo wa mazingira ndani na pembezoni mwa Ziwa kwa kuzuia na kudhibiti vyanzo vya uchafuzi kutoka viwandani na kwenye shughuli za kibiashara kwa kutumia mbinu n ateknolojia mbalimbali za uzalishaji bora.
Hadi sasa viwanda na shughuliza kibiashara zipatazo 63 ndani ya Bonde upande wa Tanzania zimepata mafunzo kuhusu ufanisi wa matumizi ya rasilimali na upunguzaji wa uchafuzi yaliyoendeshwa na kituo cha Uzalishaji Bora na Hifadhi ya Mazingira (CPCT) na 20 miongoni mwao zimefanya tathimini ya uzalishaji bora (Resource Efficient & Cleaner Production Assessments) kwenye maeneo yao na kutambua fursa mbalimbali za kuboresha shughuli zao.
Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akitambulishwa kusanyikoni. |
Wadau kwenye hafla. |
Kuna aina tano za tuzo ambazo ni:- (i) tuzo ya kupunguza taka ngumu (Solidi waste reduction),
(ii) Tuzo ya kupunguza maji taka (Waste water reduction)
(iii) Tuzo ya ufanisi wa matumizi ya maji (Water use management),
(iv) Tuzo ya ufanisi katika matumizi ya nishati (kupunguza hewa ukaa)
(v) Tuzo ya mshindi wa Jumla (Overall Cooperate Award).
Lengo kuula Tuzo hizi (RECP Awards) ni kujenga kichocheo na mfumo wa kuwatambua wanaofanya vyema katika shughuli za viwanda na biashara kwa kuzingatia ufanisi wa rasilimali na kupunguza uchafuzi wa mazingira kama namna ya kuongeza tija katika uzalishaji, kupunguza uzalishaji wa taka, kuboresha usalama na afya kazini na kuongeza ushindani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.