Ndege ya abiria ya Iran ilijipata katika barabara ya umma baada ya kuteleza katika barabara ya uwanja wa ndege ilipokuwa ikitua.
Abiria wawili kati ya 136 waliokuwa wakiabiri ndege hiyo walipata majeraha ya miguu kufuatia kisa hicho katika mji wa Mahshahr, kulingana na maafisa wa afya.
Ndege hiyo ya kampuni ya Caspian iliondoka mjini Tehran . Matairi yake hayakujitokeza kabisa wakati ilipotarajiwa kutua.
- Ndege kubwa zaidi ya injini mbili yapaa
- Ndege ya Ukraine iliyoanguka Iran ilitaka kusitisha safari
- 176 wafariki katika ajali ya ndege Iran
Picha za abiria waliokuwa wakitoka katika ndege hiyo zilichapishwa katika mitandao ya kijamii.
Runinga ya serikali ilinukuu maafisa wa usafiri wa angani wakisema kwamba rubani aliishusha ndege hiyo kuchelewa hivyobasi akakosa barabara ya ndege.
Ripota mmoja ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo alisema kwamba matairi ya nyuma ya ndege hiyo yaliharibika na kwamba ndege hiyo iliteleza bila matairi yake.
Msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani Reza Jafarzadeh aliambia chombo cha habari cha Isna news kwamba ndege hiyo iliteleza kutoka katika barabara yake siku ya Jumatatu alfajiri .
Aliongezea kwamba uchunguzi unaendelea.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.