ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 7, 2018

REFA MKENYA ALIYETEULIWA NA FIFA KUSIMAMIA KOMBE LA DUNIA 'ANASWA NAKAMERA AKIPOKEA RUSHWA'


Takriban maafisa 100 wa kandanda katika eneo la Afrika Magharibi na Kenya walipatikana katika kamera wakipokea fedha katika operesheni kali.

Ni miongoni mwa upelelezi wa miaka miwili uliofanywa na mwandishi wa Ghana mwenye utata Anas Aremeyaw Anas. Kipindi cha BBC Africa Eye kimepata kanda za video za kipekee katika makala yao ya mwisho.

Katika kisa kimoja naibu refa kutoka Kenya anayeelekea Urusi kuchezesha dimba la dunia kutoka Kenya alikubali dola 600 kutoka kwa mtu aliyejifanya kuwa afisa wa shirikisho la soka la Ghana.

Fifa inasema kuwa refa huyo kwa Jina Aden Range Marwa , ambaye ni mmojawapo wa marefa walioteuliwa na Fifa kushiriki katika kombe la dunia nchini Urusi , hataelekea tena Urusi baada ya kupatikana akipokea zawadi ya $600.

Marwa alipewa fedha hizo na mwandishi mpelelezi aliyejifanya kuwa afisa mkuu wa timu moja kuu ya Ghana. Hatahivyo refa huyo amekana kufanya makosa yoyote.

Mwanachama wa baraza la Fifa nchini Ghana Kwesi Nyantakyi , ambaye ndiye afisa wa pili kwa uwezo katika soka ya Afrika , pia alipatikana na operesheni hiyo kali.

Alionekana akipokea $65,000 kutoka kwa mwandishi mpelelezi aliyejifanya kuwa mwekezaji katika soka ya Ghana.

Nyantakyi amekataa kutoa tamko lolote. Kwa jumla zaidi ya marefa 100 na maafisa wakuu walipatikana katika kamera wakichukua fedha kinyume na sheria za Fifa na GFA .

Makala hiyo iliofanywa na mwandishi aliyezua utata Anas Aremayaw Anas imezua maswali makali kuhusu hatma ya mchezo wa kandanda wenye ushabiki mkubwa barani Afrika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.