ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 8, 2018

SERIKALI YASEMA BARUA WALIOANDIKIWA KKKT NI BATILI.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema barua iliyoandikwa na wizara hiyo na kulitaka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) kuufuta waraka wa Pasaka ni batili.

Dk Nchemba ameyasema hayo Leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari amesema taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni batili na siyo maelekezo ya serikali au wizara.

“Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo,” amesema.

Pia Dk Nchemba amesema amefuatilia barua hizo na kuona zina mkanganyiko wa anuani.

“Viongozi wa dini wasiwe na taharuki na taarifa hizo, hazina baraka za Serikali. Wasisite kuwasiliana na Serikali kujua uhalali wake.” Amesema.

Pia Dk Nchemba amesema waraka wa viongozi wa dini uliotolewa miezi iliyopita ni jambo lililopita na hivyo akawataka viongozi wa dini waendelee na kazi zao.

Dk Nchemba amewataka viongozi wa dini kuendelea na kazi zao. “Nchi yetu ni moja na tunaishi kwa taratibu tulizojiwekea na tuna madhehebu mengi.” Amesema na kuongeza: “Wengine wameliona jambo hilo kama ajenda. Wananchi wawe makini, wasiwafuate watu hao wanaotaka kuwagawa.”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.