
Wengine ni Haji Mkweda (21), ambaye alijeruhiwa mguu wa kulia, Judhith Madaraka (26), aliyechomwa kisu kwenye titi lake la kushoto na mkono wa kushoto, Ivory Mchimba (26), aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni. Majeruhi wote ukiondoa wabunge hao na Waziri, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.
Kamanda Barlow alisema katika vurugu hizo magari matatu likiwemo la Kiwia yaliharibiwa.

Polisi ilipata mapema taarifa za tukio hilo lakini ilichelewa kufika kutokana na eneo hilo kuwa lenye mawe na milima hivyo kufika wakati tayari wabunge wameshajeruhiwa vibaya na mali hizo kuharibiwa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mabina amekana wafuasi wake kuhusika na uvamizi huo dhidi ya wabunge hao, akidai kwamba pengine wabunge hao walikutana na wahuni au majangili wakawavamia na kuwashambulia kwani mazingira ya usiku namna hiyo huwezi kuamini kwamba CCM wamefanya shambulio hilo nakuwataka wabunge hao wahojiwe zaidi walikwenda kufanya nini maeneo hayo nyakati hizo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.