Maamuzi hayo yamekuja kupitia kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa muda sasa ikihusiana na uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo katika kusikiliza kesi hiyo upande wa Lema uliwakilisha mashahidi wanne.
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kupitia jaji Gabriel Rwakibarwa wa Sumbawanga imemvua Ubunge bwana Godbless Lema kwa madai kwamba kulikuwa na chembechembe za udhalilishaji wa matusi, kidini, kijinsia na kikabila, hivyo wananchi wa jimbo hilo wanalazimika kufanya uchaguzi tena. Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi wa 2010 Godbless lema aliibuka kwa ushindi wa kura 56,569 wakati mpinzani wake Dr.Batilda Buriani alipata kura 37,460.
Hata hivyo, Lema hakuondolewa haki ya kugombea ubunge huo tena na kwa taarifa za watu wa karibu, Lema hatakata rufaa mahakamani juu ya hukumu ya kesi hiyo, bali atakata rufaa kupitia kura ya wananchi wa Arusha Mjini, hivyo tutarajie uchaguzi mpya hivi karibuni.
Tanzania, nchi ya uchaguzi kila uchao...mmmmmmh!
Tupe maoni yako
Kupitia mpango huu ndiyo kwanza CCM wamejichimbia kaburi na hali yao ya umauti, Chadema tutasonga kwa nguvu za Mungu.
ReplyDeleteHaki ya mtu kamwe haizurumiki watafanya fitina zote sanasana watajimaliza tu kwa kujinyonga na kamba zao wenyewe yaani kurudia kura bora walioamua kujivua magamba chukuwa chako mapema
ReplyDelete