ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 5, 2012

KUNDI LA WATU 1000 WAVAMIA MGODI GEITA

MGODI wa dhahabu wa Geita (GGM) leo umechafuka baada ya kundi la wachimbaji wadogo zaidi ya 1000, kuvamia mgodini humo kwa lengo la kuchukua mawe ya dhahabu, na kuteketeza gari moja kwa moto huku watu watano wakijeruhiwa.

Inasemekana watu hao waliovamia ni wachimbaji wadogowadogo ambao wamekuwa wakihangaika kutokana na maeneo waliyoaidiwa na waziri Ngereja kutengwa kwa ajili yao kukosekana, hivyo kila wanapokabiliwa na hali ngumu wamekuwa wakivamia mgodini kuchukua mawe ili nao wakajitafutie mali.

HABARI KUTOKA NDANI.

Hali imekuwa tete sana katika mji wa Geita na hata hapa mgodini, FFU wamemwagwa kwa wingi sana kutoka Mwanza na sasa wenzetu walioko Geita mjini wanasema hali kidogo inaanza kurudi katika hali yake ya kawaida. Magari yote madogo yanayotumiwa na supervisors wanaokaa mjini yamezuiwa kwenda mjini, hivyo watumiaji wake nao wametakiwa na uongozi wa mgodi kutumia mabasi, ambayo nayo yanasafiri kwenda mjini kutoka mgodini kwa escort ya polisi (FFU). Wafanyakazi hapa mgodini wameshikwa na wasiwasi mkubwa, na wengi wamekuwa wakifikiri kuwa huenda wakafanyiwa fujo pindi wafikapo mjini na nguo za kazini zenye reflectors.

Ni hali ambayo haijawahi kutokea nafikiri toka mgodi huu umeanza, jambo linaloashiria kuwa kuna tatizo mahali flani ambalo linahitaji kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo na mamlaka zinazohusika. Mambo haya yanayotokea hapa yamekuwa yakitokea kwenye migodi mingine, hususani mgodi wa North Mara, na kila mtu anakumbuka ni kwa jinsi gani mgogoro ule ulivyochukua sura mbalimbali zisizopendeza zilizopelekea vyombo vya usalama na wanasiasa kulaumiana. Natumaini vyombo vya habari vitaendelea kutujuza mengi leo usiku na hata kesho kwenye magazeti yetu maana natumaini waandishi wa habari watakuwa wamewasiliana na mamlaka husika na hivyo kujua mengi kuhusiana na mgogoro huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.