JESHI la Wananchi Tanzania na Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Jumanne ya Tarehe 24 Mei 2022 limekabidhiwa Bendera ya Taifa tayari kuianza safari kuelekea nchini Uganda, kushiriki mazoezi ya pamoja ya Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Meja Jenerali wa Jeshi la Wananchi Tanzania Athony Suguti ndiye aliyelikabidhi bendera kwa jeshi hilo katika viwanja vya Kikosi Cha Usafirishaji Nyegezi jijini Mwanza. Tanzania imetuma askari wake 299 kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Uganda. Na kwa mujibu wa Mkuu wa kikundi cha Tanzania kinachokwenda kushiriki zoezi hilo la Ushirikiano Imara nchini Uganda Brigedia General Charles James Ndiege amesema mazoezi hayo yanayoshirikisha Zaidi ya askari na raia elfu moja kutoka Tanzania, Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, DRC Kongo na wenyeji Uganda ni pamoja na operesheni za kuunga mkono amani, usimamizi wa maafa, vita dhidi ya ugaidi na uharamia. Mazoezi hayo yalianza kwa mara ya kwanza mwaka 2004 kwa lengo la kuimarisha uwezo wa majeshi ya nchi wanachama katika kulinda amani ili kuzuia matukio chungu katika eneo hilo kama tukio la mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.