Amesema kuwa mikakati iliyopo kwa sasa ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, ni nchi zilizo katika jumuiya hiyo kuendeleza mipango ya kutokomeza tatizo hilo kwa ushirikiano wa karibu kwa nchi zilizo mwanachama ambazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi kwa kutoa semina, kongamano na mbinu zingine ambazo zitaweza kuwaelimisha wananchi ili kubadirisha tabia zao ambazo zinaleteleza maambukizo ya ugonjwa huo.
Dk. Mrisho amesema kuwa maambukizo mengi katika miongoni mwa wananchi walio katika Jumuiya hiyo yanatokana na ngono zembe miongoni mwa jamii, madereva wa magari makubwa yanayosafirisha bidhaa baina ya nchi hizo, wafanyakazi katika mabaa na sehemu zingine za starehe pamoja na maeneo yenye mlundikano wa watu wengi ambao huleteleza muingiliano usio rasmi.
Ameongeza kuwa endapo nchi zilizo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki zitafanya kazi kwa pamoja katika kutokomeza janga hilo, hadi kufikia mwishoni mwaka 2012, ugonjwa huo utakuwa umetokomezwa kabisa au kupungua kwa kiasi fulani iwapo jamii katika nchi husika itajikita katika kuthibiti maambukizo hayo.
Hata hivyo, Dk. Mrisho amesema kuwa nchi zilizo katika jumuiya hiyo kwa kupitia taasisi zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo zitakutana mara kwa mara ili kubadirishana uzoefu wao, itakuwa ni rahisi kutambua matatizo yaliyo katika nchi husika na kuweza kushirikiana katika kuyatatua ili kuweza kuwa na malengo ya pamoja katika kubambana na ugonjwa huo.
Mkutano huo ambao umeanza Machi 16 utahitimishwa kesho Machi, 18 ambapo kwa mujibu wa Dk. Mrisho ambaye ni mwenyeji katika mkutano huo, wajumbe wataweza kutoa maamuzi ya jumla ambayo yatalenga kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.