Waziri Wa Maji Mh. Mark Mwandosya leo amefungua wiki ya Maji mjini hapa kwa kuzindua mradi mkubwa wa Maji taka katika eneo la Butuja Wilayani Ilemela Mwanza.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mwanza (MWAUASA) Bw. Mashaka Sitta alisema kuwa mradi huo utakaogharimu karibu Billioni 29 ulibuniwa mwaka 2002 na kuanza kutekelezwa tangu mwaka 2009.Alieleza kuwa miradi itakayojumuisha katika mradi huo ni pamoja na ujenzi wa bomba kubwa la kipenyo cha mm 700 kwa umbali wa mita 140,ujenzi wa mabwawa mapya matatu, ukarabati wa mabwawa kumi ya zamani, ujenzi wa matanki mapya ya kuhifadhia Maji taka pamoja na ununuzi wa vifaa vya maabara.
‘’ Tunatarajia kuwa kukamilika kwa mradi huu itatuwezesha kujenga pia mtandao wa Maji taka kwa kilomota 24, kujenga mashimo ya maji taka (manhole chambers) zipatazo 880 itakayounganisha karibu nyumba 5000 kwenye mtandao wa majitaka’’ alisema Mkurugenzi huyo.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Mh Waziri alisisitiza umuhimu wa kutunza miradi hii kwani Wafadhili wanatumia fedha nyingi kugharamia miradi hii. ‘’Nisingependa baada ya ufunguzi huu wa leo, tuwaombe tena Wafadhili kutukarabatia miundominu yetu nitashukuru kama kutakuwa na kazi ya mamna hii katika Nchi moja ya jirani basi kazi hiyo ifanywe na MWAUSA’’ alisisitiza Mwandosya.
Pamoja na uzinduzi huo Mh.Waziri alipokea pia magari 4 ya kubebea maji taka yatakayotumika na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka jiji Mwanza.Sherehe ya UzinduzI wa mradi huu mkubwa maji taka ulihudhuriwa pia na Mwakilishi mkuu wa Jumiya ya Ulaya hapa Tanzania Balozi Tom Clarke, Balozi Mdojo wa Ujerumani hapa Nchini pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya maendeleo ya Ujerumaini (KWF) Dr Wolfgang.
Maadhimisho ya wiki ya Maji yanafanyika katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza na yatafikia kilele chake tarehe 22 Machi kwa kufungwa rasmi na Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Gharib Bilal.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.