Ibada ya kuuaga mwili wa Askofu Alpha Francis Mohamed Imefanyika leo katika kanisa la anglikana Arusha Christ Church Cathedral Diocese of Mountain Kilimanjaro.
Jaji mkuu mstaafu Barnabas Samata akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu baba askofu Alpha Francis Mohamed.
Mchungaji Kajembe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa baba askofu.
Askofu Alpha alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa dayosisi ya mtakatifu Kilimanjaro, na katika maisha yake amevisaidia vikundi mbalimbali vya akina mama katika kuanzisha miradi na kuwezesha kusomesha watu mbalimbali.
Muimbaji wa muziki wa injili Betrice Muhone ni mmoja wa waliohudhuria ibada hiyo.
Kwaya ya Upendo kutoka st.James Arusha katika heshima za mwisho.
Mungu wa rehema nyingi, Baba wa Bwana Yesu kristo uliye ufufuo na uzima, ambaye kila amwaminiye yeye, ajapokufa, ataishi, na kila mwenye kuishi ndani yake na kumwamini hafi milele.
Watumishi wa mungu katika picha ya pamoja na mwili wa marehemu baba askofu Alpha Francis Mohamed aliye zaliwa tarehe 22/nov/1941 na kufariki dunia tarehe 14/march/2011, Mwili wake umesafirishwa leo kwa ndege ya Precision air kuelekea mkoani singida kwa mazishi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana lihimidiwe.
ENDORO WATER FALLS, MAAJABU MENGINE NGORONGORO
-
Mbaraka Mwinshehe aliwahi kuimba akiisifia Morogoro na jinsi maji
yanavyotiririka kutoka milimani.
Mwinshehe angekuwa hai pengine angefika maporomoko ...
Rais Museveni atangazwa mshindi wa uchaguzi Uganda
-
Tume ya uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Kaguta Museveni kama
mshindi wa uchaguzi uliofanyika Alhamisi wiki hii, akiwa na jumla ya kura
7,946...
0 comments:
Post a Comment