NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hii leo amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi km 3) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75. Mhe. Rais Samia amekagua Daraja hilo ambalo Ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Februari, 2024. Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Misungwi Michael Masanja Smart akasimulia jinsi ujenzi wa daraja hilo walivyokuwa wakilichukulia kama hadithi za 'Abunuasi' lakini imekuwa kinyume na hatimaye ndoto hiyo inakwenda kutimia kupitia Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. #samiasuluhuhassan #mwanza #kaziiendeleeTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.