NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku nne huku akisisitiza umoja katika ujenzi wa Taifa. Akisalimia na umati wa wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kumpokea eneo la uwanja wa Ndege (Air Port Mwanza) katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, Mkuu huyo wa nchi amesema Tanzania ni nchi moja isiyogawanyika na kuwataka Watanzania kila mmoja kwa eneo lake kutimiza wajibu wa kujenga uchumi wa nchi, kisha akatia msisitizo kwa kusema "TANZANIA NI MOJA HAIUZIKI WALA HAIGAWANYIKI MIMI NI MTANZANIA"Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.