ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 16, 2023

MAMA KOKA ATEMA CHECHE MAADHIMISHO YA MTOTO WA AFRIKA

 


Na Victor Masangu,Kibaha 


Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Selina Koka amehimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri ya kuwalinda na kuwatunza watoto wao ikiwa sambamba na kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo suala la  elimu.

Mama Koka ambaye pia ni mlezi wa jumuiya ya umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mjini (UWT) ameyasema hayo leo ikiwa ni katika kilele Cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika duniani


Alisema kwamba jamii yote kwa kushirikiana na wazazi wanapaswa kubadilika kupitia siku hii na kuona umuhimu mkubwa wa kuwapa fursa sawa pamoja na ulinzi ili waweze kuishi katika mazingira mazuri.


"Siku hii ya maadhimisho ya mtoto wa afrika pia inatukumbusha sisi kama wazazi,na walezi kuwatupia macho zaidi watoto wetu katika kuwapatia fursa mbali mbali watoto wetu ikiwemo suala la fursa ya elimu pamoja na nahitaji muhimu ambayo yatawafanya watoto wapate furaha,"alisema Selina Koka.

Aidha aliongeza kuwa ana imani kwamba watoto pia wakilindwa na kupatiwa maadili mazuri yataweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwa na heshima katika jamii na kuweza kutimiza malengo na ndoto zao waliojiwekea.


Katika hatua nyingine aliahidi kuweka mikakati madhubuti kwa kushirikiana na jumuiya ya umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mjini katika kuwasaidia kwa hali na mali watoto yatima pamoja na wale ambao wanaishi katika mazingira rafiki kwa kuwasaidia mahitaji yao mbali mbali.


" Mimi nitaendelea kushirikiana bega kwa bega na wazazi pamoja na walezi katika kuwalinda na kuwatunza watoto wetu na  kitu kikubwa zaidi ninkuwapatia malezi bora na kuachanyana kabisa na na tabia ya kuwatumikisha kazi ngumu n vitendo vya ukatili hii sio nzuri hata kidogo kikubwa wote tushikamane,"alisema Selina Koka.

 Maadhimisho ya siku ya mtoto wa afrika ufanyika kila mwaka ifikapo Juni 16 ambapo kwa mwaka huu katika ngazi ya Mkoa wa Pwani yamefanyika katika Wilaya ya Kibiti na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.