ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 15, 2023

MV MWANZA KUKUZA UCHUMI

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ameridhika na maendeleo ya ujenzi wa meli ya MV. Mwanza, ambayo itasaidia kukuza biashara mkoani Mwanza, mikoa jirani na nchi jirani. Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba mizigo hadi tani 400 kwa mara moja, itasaidia kwenye usafirisaji wa mazao katika nchi za Maziwa Makuu na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo. Aidha, Rais ameahidi kurudi kuizindua MV. Mwanza itakapokamilika na kuwataka Watanzania kuendelea kutunza amani na utulivu, kwani ndio chachu kwenye biashara za Kimataifa na uwekezaji. MV Mwanza itakuwa na madaraja sita ambayo ni VIP itakayokuwa maalum kwa viongozo wa kitaifa ambapo watakuwa wanakaa watu wawili tu pamoja na viongozi wa kitaifa wa nchi jirani kama watapata kibali cha kusafiri na meli hiyo. Daraja la VIP ambalo litabeba watu mashuhuri sehemu hii itakuwa na watu wanne yaani vyumba vinne, daraja la kwanza litakalokuwa na watu 60, daraja la biashara litakalokuwa na watu 100 daraja la pili litakalokuwa na watu 200.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.