NA ZEPHANIA MANDIA G.SENGO TV
Idara ya uhamiaji mkoani Mwanza imewataka raia wote wa kigeni wanaoishi katika jiji la Mwanza kuhakikisha wanajiorodhesha katika daftari la orodha ya wageni wanaoishi hapa nchini ambayo yametolewa katika ofisi za watendaji wa kata na mitaa katika jiji hilo.
Agizo hilo limetolewa na Afisa uhamiaji mkoa wa mwanza, Naibu kamishna wa uhamiaji, Paul Eranga wakati akitoa elimu ya uraia na wajibu wa viongozi wa serikali katika kukabiliana na wimbi kubwa la wahamiaji haramu kwa wenyeviti, watendaji wa kata na mitaa zaidi ya 60 kutoka kata 18 za wilaya ya nyamagana mkoani Mwanza ambapo amesema raia yeyote wa kigeni ambaye atakaidi agizo hilo atachukuliwa hatua zakisheria kwa atakayebainika.
Aidha naibu afisa uhamiaji wa mkoa huo na afisa uhamiaji wa wilaya ya nyamagana moses mutash wamewataka watendaji na wenyeviti hao kufuata sheria na taratibu zinazoelekeza hatua za kufuatwa katika kufanya maamuzi na kuidhinisha maombi ya uraia ambayo yanawasilishwa kwao na raia wa kigeni.
Kwa upande wao baadhi ya watendaji hao wametoa hisia zao kuhusiana na elimu ya uraia na wajibu wao katika kukabiliana na wimbi kubwa la wahamiaji haramu katika maeneo yao na kuomba ushirikiano kutoka kwa maafisa uhamiaji punde wanapowabaini wahamiaji haramu katika maeneo yao ukizingatia jiji la Mwanza ni lango kubwa kwa nchi jirani UGANDA, RWANDA, BURUNDI, DR CONGO NA KENYA.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.