NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, ameziagiza halmashauri zote
mkoani hapa kuhakikisha asilimia tano za wanawake na vijana, zilizokuwa
zikitolewa katika makundi hayo, zianze
kutolewa kwa wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) ambao wamesajiliwa na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA)
Mongella ametoa agizo hilo wakati wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho
maalumu kwa wafanyabiashara ndogo ndogo jijini Mwanza waliojiunga katika
vikundi mbalimbali vya wajasliamali, ambapo amesema atashangazwa kuona
vikundi ambavyo sio rasmi vikipewa
mikopo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Charles Kichere,
amewaomba wafanyabiashara wadogo wadogo (Machinga) kujiunga katika vikundi
vidogo vidogo ili waweze kunufaika na mikopo mbalimbali inayotolewa na Taasisi
za kifedha.
Naibu Kamishna wa kondi za ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Michael Mhoja, amesema mamlaka hiyo tayari imesajili vikundi 30 vya
wafanyabiashara ndogo ndogo vyenye jumla ya wafanyabiashara 1,110 huku akidai
mpango wao ni kusajili vikundi 130.
Nae Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire akatoa neno kwa wajasliamali
hao huku baadhi ya wafanyabiashara hao nao wakazungumzia zoezi hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.