Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa Kahawa Wilayani Muleba wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Muleba kusini Mhe. Prof Anna Tibaijuka kabla ya mkutano na wadau wa Kahawa Wilayani Muleba wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akimakabidhi muongozo wa ujenzi wa viwanda Mkuu wa Wilayani ya Muleba Mhe Richard Ruyango mara baada ya kuwasili Wilayani humo kwa ajili ya mkutano wa wadau wa Kahawa wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt Consolata Ishebali.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wadau wa Kahawa Wilayani Muleba wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018.
Na
Mathias Canal-WK, Muleba-Kagera
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt
Charles Tizeba Jana 12 Julai 2018 ameitaka Benki ya CRDB kulipa haraka malipo
ya fedha za Ushirika za Chama Kikuu cha Kagera (KCU) kulingana na hatma ya kesi
iliyokuwa mahakamani mwaka 2003 ambapo wakulima walikuwa wakikatwa kiasi cha
shilingi 10 kwa kila kilo moja ya Kahawa ili kujenga mfuko wa Mazao kwa miaka
mitatu kuanzia mwaka 1990 hadi 1993.
Dkt Tizeba ametoa agizo hilo
wakati akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha wadau wa Kahawa Wilayani
Muleba ikiwa ni siku ya tatu ya ziara ya kikazi mkoani Kagera iliyoanza Juzi 10
Julai 2018 na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe
Charles Mwijage.
Swala la madai hayo katika
mkutano huo liliibuka baada ya baadhi ya wakulima kuonyesha vitabu vya mfuko
huo ambapo makato hayo ya shilingi 10 kwa kilo kwa kipindi cha miaka mitatu
jinsi ambavyo yalikuwa yakifanyika.
Madai ya wakulima hao yamekuwa
yakilalamikiwa kwa kipindi kirefu na kuchangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa
imani ya wakulima kwa chama kikuu cha ushirika Kagera (KCU).
Chanzo cha kesi hiyo ni baada ya
Benki ya CRDB kuzuia fedha za malipo yaliyotokana na mauzo ya Kahawa ili
kulipia deni la msimu wa mwaka 1997/1998.
Hukumu ya kesi iliyotolewa
tarehe 28 Octoba 2009 na mfuko wa Mazao wa wakulima Mkoani Kagera kupewa
tahfifu ulizoomba ambapo tangu wakati huo Benki ya CRDB iliweza kulipa fedha za
mfuko ilizochukua kiasi cha shilingi milioni 525 na fedha zilizobaki bado
hazijalipwa kwa kisingizio cha kuwa na nia ya kukata rufaa ambayo bado
haijakatwa ambapo hata hivyo hawawezi kukata rufaa kutokana na muda kuwa
umepita.
Dkt Tizeba alisema kuwa Jumla ya
madai hayo sambamba na riba ni shilingi Bilioni sita za kitanzania huku
akisisitiza kuwa Benki hiyo ya CRDB inapaswa kuwa mfano wa Benki zingine nchini
hivyo kushindwa kuwalipa wakulima kwa wakati ni kushindwa kwenda na serikali ya
awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli.
Wakati huo huo Waziri Tizeba
aliagiza Halmashauri zote nchini zinazolima Kahawa kusimamia ukusanyaji wa
Kahawa kwenda vya Msingi (AMCOS) kwani kutokana na usimamizi huo ndio hupata
ushuru wa Halmshauri.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.