Akijibu swali la mtangazaji wa Jembe FM, Jackson Joseph aka JJ, kupitia kipindi cha HOT STAGE kinachoruka kila siku za jumatatu hadi alhamisi saa moja usiku hadi saa tatu, kwamba '....ni Ujumbe gani anao wapa wasanii wanavuma sasa kwenye game' Profesa amesema " sasa hivi hatutizami tena maslahi ya Profesa Jay, tunatizama maslahi ya muziki wetu, tumeleta mapinduzi makubwa kwenye muziki huu kwa nyimbo kama Chemsha bongo kuwaaminisha wazazi kuwa huu muziki si wakihuni ingawa kunawahuni wachache huu muziki wanaufanya.
Kisha akaongeza "Lakini pia tumetaka kuwaambia wazazi kwamba muziki unaweza kuleta ajira, wengi mmeona kwamba wasanii wengi wanajiajiri na kuajiri watu wengi katika sanaa na tasnia ya muziki..........."Nawashukuru wasanii chipukizi kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa, akina Joh Makini wako wengi wanao Re-Present kwa kweli Aika, Navy Kenzo wanafanya vizuri kwa kweli kuupeleka muziki kwenye levo nyingine lakini wanahitaji sapoti inabidi tushambulie kama Barcelona, tunashambulia pamoja tunakaba pamoja"
ZAIDI BOFYA UPATE KUSIKILIZA KILICHOTOKEA.Aidha Prof Jay amedai kuwa Singeli ni muziki unaoweza kulipeleka taifa hili mbali kwani unaojumuisha ladha nyingi za asili ya Tanzania .
“Sisi watanzania tumekuwa na muziki ambao haueleweki, hata hip hop tunayoifanya inayoweza kumuonesha huyu ni mtanzania ni Kiswahili tu,” amesema Jay.
“Nimefanya hip hop singeli kwaajili ya kuupeleka muziki huo mbali lakini pia kuitengeneza hip hop tofauti. Kuliko kuwakopi akina Lil Wayne wanafanyaje basi tufanye muziki ambao tutakopi muziki wa nyumbani,” ameongeza.
“Nadhani ni muda sasa hivi wasanii wa hip hop kutanua, wasikopi vya Marekani, wako vya Tanzania ili kuifanya hip hop yetu ibadilike kila siku.”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.