ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 27, 2013

MWANZA HUDUMA YATOA MIFUKO 200 YA SARUJI KUBORESHA VYOO VYA SHULE 4 ZA MSINGI WILAYA YA NYAMAGANA

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga wa pili kulia pamoja na Mkurugenzi wa Duka la vifaa vya ujenzi la Bw. Zuri Nanji wa kwanza kulia wakikabidhi mifuko 50 kwa uongozi wa shule ya msingi Butimba Mazoezi  A na B iliyopo Kata ya Butimba kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo. 
 MKUU wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga jana alikabidhi jumla ya mifuko 200 ya  saruji kwa shule nne za msingi katika Kata nne za Wilaya hiyo ikiwa ni mkakati wake wa kuchangia, kuhamasisha mendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa vitendo.

Konisaga ambaye amekuwa akihamasisha mkubwawa maendeleo na kuhakikisha kero mbalimbali za kijamii zinatafutiwa ufumbuzi wa haraka kwenye sekta zote ambapo katika msaada huo alioukabidhi kwa lengo la kupunguza upungufu wa matundu ya vyoo kwenye baadhi ya shule hizo zinazokabiliwa na changamoto hiyo kutokana na wingi wa wanafunzi.

“Msaada huu wa saruji mifuko 200 umetolewa kwangu na mfanyabiashara maarufu Jijini Mwanza Zuri Nanji maarufu kwa jina la ‘Mwanza Huduma’ ambaye alikuja ofisini kwangu na kuniahidi kunisaidia kwenye sekta ya Elimu lakini kwa shule za msingi na eneo alilopendekeza ni kwenye ujenzi wa vyoo ili kusaidia kuongeza matundu ya vyoo jambo ambalo litasaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi wakihitaji kujisaidia”alisema

Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba kutokana na msaada huo aliamua kuugawa kwenye shule za msingi nne kati ya 81 zilizopo katika Wilaya hiyo ambapo shule zilizonufaika na msaada huo ni Butimba Mazoezi  A na B iliyopo Kata ya Butimba, Ibanda iliyopo Kata ya Mkolani, Igogo B iliyopo Kata ya Igogo na Igoma iliyopo Kata ya Igoma.
Pamoja na makabidhiano hayo yaliyofanywa shule ya msingi Butimba imeendeleza juhudi zake za ujenzi wa vyoo ili kupunguza makali ya changamoto iliyopo.

Msafara wa Mkuu wa wilaya ya Nyamagana na wadau wake ukirejea toka kwenye ukaguzi shule ya msingi Butimba Mazoezi  A na B iliyopo Kata ya Butimba..

Konisaga pia alipata fursa fupi ya kuzungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Butimba Mazoezi  A na B iliyopo Kata ya Butimba.

Makabidhiano ya Mifuko 50 ya saruji kwa shule ya Msingi Mkolani.

Waalimu na wanafunzi shule ya msingi mkolani.

Saruji ikishushwa shule ya msingi Mkolani.

Mifuko 50 ya Saruji kwa shule ya msingi Mkolani. 

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na waalimu, wanafunzi na uongozi wa kamati shule ya msingi Igogo ambapo alikabidhi mifuko 50 kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo.

Vyoo vya shule ya msingi Igogo ambavyo tayari vimejengwa. 

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akikabidhi Naibu Meya John Minja mifuko 50 ya saruji huku akishuhudiwa na viongozi wa kamati na waalimu wa shule ya msingi Igogo B iliyopo Kata ya Igogo wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo.

Kabla ya makabidhiano kwa shule ya msingi Igoma waalimu na wanafunzi walikutanishwa katika ukumbi wa shule hii kwaajili ya kupata changamoto zilizopo.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (wa pili kutoka kushoto) akikabidhi mifuko 50 kwa uongozi wa shule ya msingi Igoma kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya shule hiyo.

“Hali ya vyoo kwenye shule hizi si nzuri sana hivyo Mudau huyu ‘Mwanza Huduma’ ameguswa na hali hiyo na kuonyesha umuhimu wake kutokana na shughuli zake nyingi kuzifanyia Wilayani kwetu kweli ni mfano wa kuigwa kwani shule hizi ni mali ya wazazi ambao wanatakiwa kuchangia uboreshaji wake ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, madawati na matundu ya vyoo” alisisitiza.

Konisaga alisema kwamba wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule za msingi  na sekondariwanao wajibu mkubwa kwa kushirikiana na walimu na kamati zao za shule hizo kuboresha miundombinu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji na Serikali kwa kuchangia fedha ili kupunguza aidha kuondoa kero mbalimbali kwenye miradi ya maendeleo inayotoa huduma za kijamii kwenye sekta zote kwenye maeneo yao.

“Viongozi wa serikali ni kusimamia ulinzi na amani ya wananchi na kuwahamasisha pia kuchangia miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji na serikali Kuu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ili kuwawezesha kupatiwa huduma bora kama inavyokusudiwa na wananchi kuwaepuka wanasiasa wanaowahamasisha kutochangia miradi hiyo eti ni jukumu lake hao hawafai  na wasiwaunge mkono”alisema Mkuu huyo.

Konisaga aliwataka viongozi wa Kamati za shule hizo zilizokabidhiwa msaada huo kuacha tabia ya kuweka mafundi na kuwaacha wakichakachua na kufanya ujenzi hafifu na kusababisha majengo hayo kuwa chini ya kiwango na hata kuharibika kwa wakati mfupi jambo ambalo limekuwa likiwakatisha tamaa baadhi ya wadau, wafanyabiashara na wafadhili kuendelea kuchangia tena kwenye miradi mbalimbali ya kijamii.

Naye kwa upande wake Zuri  Nanji ‘Mwanza Huduma’ alisema kwamba hali ni mbaya sana kwenye shule za msingi ambapo kuna watoto wengi (wanafunzi) ambao kutokana na matundu ya vyoo kuwa machache husababisha wanafunzi hao kujisaidia holela na kuharibu mazingira na kuwa hatarishi kwa afya zao ikiwemo kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza hali iliyomfanya kusaidi kwa kutoa msaada huo.

“Nitaendelea kuwa mdau wa  kuchangia saruji na vifaa vingine vya ujenzi kwenye shule za msingi na sekondari ili kuhakikisha juhudi za kushirikiana na Jamii na kuiunga mkono serikali kutoa huduma kwa wananchi inatekelezwa kwa wakati kupitia pia sekta binafisi  ili kuwapatia huduma zinazositaili kwenye maeneo yao bila kuwabagua kutokana na tofauti ya kipato”alisema


Kwa mujibu wa maelezo ya kitaalamu ya mafundi wa Ujenzi wa majengo na Mwanza Huduma alieleza kuwa kila Shule hizo zilizopatiwa kila moja mifuko ya saruji 50 yenye uwezo wa kutoa tofari 1400 kwa kila mfuko mmoja wa kilo 50 unaouwezo wa kutoa tofari 28 hadi 32 na kuhitaji maji mengi hali inayoimarisha kuta za majengo na kuwa imara na bora baada ya kukamilika huku vyoo vya matundu 8 vya kisasa vikitumia tofari 450 tu .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.