ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 29, 2015

TFF YAUTOSA UWANJA WA NYAMAGANA?

HATIMAYE ndoto za wakazi wa Manispaa ya Bukoba kufaidi michezo ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao zitatimia sasa, baada ya Serikali nchini kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania TFF kuruhusu nyasi zilizokuwa zimekwama bandarini kwa muda mrefu kuwasili katika uwanja wa kaitaba.

 Viwanja vya Nyamagana (Mwanza) na Kaitaba (Bukoba mkoani Kagera) viko katika mchakato wa kuwekewa nyasi bandia kwa msaada wa Fifa na Serikali. 

Lakini wakati uwanja wa Kaitaba wa mkoani Kagera ukipokea nyasi zake uwanja wa Nyamagana wenyewe bado nyasi zake ziko bandarini suala ambalo Chama cha soka mkoa wa Mwanza MZFA kupitia kwa katibu wake Nassib Mabruk amesema kuwa tayari wamewakumbusha TFF ili suala la Nyamagana nalo lipatiwe ufumbuzi ukizingatia umuhimu wa uwanja  huo mkongwe jijini Mwanza katika Maendeleo ya Michezo hapa nchini.

Nyamagana ndiyo ilikuwa plani ya kwanza, baadaye ikifuatia Kaitaba. Swali ni je 'Kwanini Kaitaba Kwanza na siyo Nyamagana?'

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.