Taarifa kwa vyombo vya
habari.
Yah:
Timu ya Taifa ya ngumi yaanza vema katika mashindano ya kimataifa kwa nchi za
Afrika Mashariki Mombasa Kenya.
Wachezaji wa timu ya Taifa
ya ngumi waliokwenda Mombasa Kenya kuwakilisha Taifa katika mashindano ya
kimataifa ya nchi za Afrika Mashariki wameanza vizuri kupeperusha bendera ya
Tanzania katika mashindano yaliyoanza leo tarehe 30/07/2015 jijini Mombasa kwa
kushirikisha nchi za Tanzania, Uganda na wenyeji Kenya, Timu hiyo yenye jumla ya mabondia
wanne na kocha Saidi Omari iliondoka juzi kwa udhamini wa viongozi wa juu wa
shirikisho la masumbwi Tanzania.
Matokeo kwa michezo
waliyocheza mabondia kutoka Tanzania yalikuwa kama ifuatavyo:-
·
Katika uzito wa 49 Kgs Gerevas
Logasian(TAN) alishindwa na Mwinyifiki Kombo wa (Kenya) kwa majaji 3.0,
·
52 Kgs. Said Hofu (TAN) alimshinda Sajabi
Yassini (Kenya) kwa majaji 2,1
·
56 Kgs Hamadi Furahisha
(TAN) alimshinda Denis Ochieng (Kenya) kwa majaji 3.0 kwa
·
60 KGS Ismail Issack
(TAN) alimshinda Mava Johnboscow (Uganda) kwa TKO
Mashindano hayo yataendelea
kesho tarehe 31/07/2015 kwa hatua ya nusu fainali na fainali za mashindano hayo
zitafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 01.08.2015 na timu kurejea nyumbani
02.08,2015.
Lengo la mashindano ni kuziandaa timu za kutoka ukanda wa
Afrika mashariki vizuri kabla ya
kwenda kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa hususani Mashindano ya
Afrika (All African Games). Shirikisho la ngumi Tanzania linawatakia mafanikio
zaidi ili kutangaza vema Tanzania kupitia mchezo wa ngumi
Habari hizi zinaletwa kwenu na
Makore Mashaga
KATIBU MKUU.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.