ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 1, 2015

WANAAPOLO WAFIA MGODINI BAADA YA KIBERENGE KUKATIKA


Image result for wanaapolo wakiwa mereraniwanaapolo wakiwa mgodini (picha na maktana)


Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog

Wachimbaji wadogo wawili (wanaapolo) wanaofiwa kufa na wengine kadhaa

kujeruliwa  katika mgodi  wa madini ya Tanzanite uliopo Mererani

mkoani Manyara .
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa tukio hilo
lilitokea  usiku wa kuamkia leo ambapo wachimbaji hao
waliangukiwa na kiberenge ndani ya mgodi huo uliopo block C unao
milikiwa na  Said Nassor (mwarabu) walipo kuwa wakiendelea na kazi.
Shuhuda huyo aliyejitambulisha kwa jina la Edison Onyango alisema kuwa
kiberenge hicho kilikatika na kuporomoka na kisha kuwaangukia watu hao
na kusababisha vifo na majeruhi.


Akizungumza kwa njia ya simu mmiliki wa mgodi huo Said Nassor

alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wamepata maiti ya
mtu mmoja na wako katika harakati za kusafirisha mwili huo kwenda kwa
ndugu zao kwa ajili ya maziko.
Hata hivyo alieleza kuwa tukio hilo ni lakawaida na kwamba polisi
walifika kwa ajili ya uchunguzi wakiwemo maofisa wa idara ya madini
ili kuchunguza undani wa tukio hilo.


www.woindeshizza.blogspot.com
“kwakweli ndugu muandishi wa habari tukio hili ni kweli limetokea

katika mgodi wangu na alijasababishwa na uzembe ila ni tukio la
kawaida kutokea na linaweza kutokea katika mgodi wowote “alisema Said
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa aliyefariki dunia
ni mtu mmoja Joseph Kimati (27).
Aliongeza kuwa waliojeruliwa katika tukio hilo ni wawili ambao
kuwa chanzo cha tukio ni kiberenge kilichokatika  na kupoteza
muhelekeo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.