KAHAMA
Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani shinyanga linamshikilia mtuhumiwa mmoja anayedaiwa kushiriki katika mauaji ya katibu wa Chama cha mapinduzi Kata ya Isagehe mauwaji ambayo yalitekelezwa mwaka jana.
Mkuu wa jeshi la polisi wilayani Kahama Leonard Nyandahu amemutaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Thomas Malenge miaka 35 mkazi wa kijiji cha Mwalugulu ambapo mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake 5 walimuuwa katibu wa CCM marehemu Daud Mbatilo.
Amesema kuwa mtuhumiwa huyo na wenzake walikodiwa na mtu ambaye bado jeshi hilo linafanya uchunguzi kwa ujira wa kupatiwa kiasi cha shilingi milioni mbili na kabla ya mauwaji hayo walipatiwa kiasi cha shilingi laki 6 na kutekeleza mauwaji hayo Desemba 03 mwaka jana.
Aidha jeshi hilo tayari limewanasa watuhumiwa wote 6na kwamba watuhumiwa watano walikwisha kamatwa na kufikishwa mahakamani lakini mtuhumiwa huyo aliyekamatwa jana mala baada ya tukioalitoloka kusikojulikana hivyo juzi alilejea akidhani walisahau na kulialifu jeshi la polisi na kufanikiwa kumutia nguvuni.
Hata hivyo Jeshi la polisi linaendekea kumhoji mtuhumiwa ili kuweza kufanikiwa kumukamata mtu aliyefadhili mauwaji hayo ili wote waweze kufikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.