Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza offa kabambe ya simu za kisasa itakayopatikana katika viwanja vya nane nane kuanzia siku ya Ijumaa tarehe 31 julai 2015, kwa muda wa siku 10.
Akiongea kuhusu ofa hiyo Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga amesema, Airtel inaendelea kuwapati wateja wake mawasiliano bora na kuwaunganisha na simu za kisasa zilizounganishwa na vifurushi vya bure vya internet katika msimu huu wa nanenane".
" Napenda kuwajulisha watanzania wote na wakazi wa Morogoro kuwa Airtel sasa tumewafikia na kusogeza huduma zetu karibu nao katika viwanja vya nanenane ambapo tutakuwa na offa nyingi ikiwemo simu za kisasa ya aina ya Airtel red itakayounganishwa na huduma za internet bure kwa mwaka mzima kwa gharama ya shilingi 75,000.
Sambamba na Airtel Red pia tunazo simu za aina nyingi ambazo ni pamoja na simu ya Huawei , Techno, Samsaung. Simu hizi zinamuwezesha mteja kuzitumia katika kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutunza rekodi zao, inatumika kama kamera ya kupiga picha pamoja na mambo mengine mengi.
Tunatoa wito kwa wateja wetu watembelee banda la Airtel katika viwanja ya Nanenane na kupata nafasi ya kununua simu hizi za kijanja kwa gharama nafuu "aliongeza Muga Airtel Smartphone Bazaar bado pia iko jijini Dar es Salaam katika maduka yote ya Airtel.
Khalikadhalika wateja wote bado pia wananafasi ya kusmatiphonica kwa kutembelea maduka ya Airtel nchi nzima.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.