James Lembeli |
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kahama mkoani Shinyanga James Lembeli amechaguliwa kutetea nafasi hiyo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA baada ya kuwashinda wagombea wengine 13.
Akitangaza matokeo msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mratibu wa zoezi hilo kanda ya Serengeti Haile Sizza amesema kati ya kura 262 zilizopigwa na wajumbe Lembeli ameshinda kwa kura 168 sawa na zaidi ya asilimia 80 ya kura zote zilizopigwa.
SAUTI YA Haile KUWAJIA PUNDE.
Lembeli ametangazwa kutetea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CHADEMA ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza kujiunga na chama hicho akitokea chama cha Mapinduzi CCM.
Mara baada ya kutangazwa kukiwakilisha chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba Lembeli amewashukuru wajumbe na kuomba ushirikiano na mshikamano ndani ya chama kwa maendeleo ya jimbo hilo.
SAUTI YA Lembeli KUWAJIA PUNDE.
Katika hatua nyingine Winfrida Mwinura amechaguliwa kuwania ubunge viti maalumu baada ya kuwashinda wagombea wengine wanne kwa kura 34 kati ya kura 77 zilizopigwa na wajumbe wa baraza la wanawake wa chama hicho(BAVICHA).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.