
Mwakilishi wa chama cha upinzani cha Rwandan National Congress, Jonathan Musonera amesema yeye binafsi ameathiriwa na amri hiyo ya serikali. Alisema serikali iliamrisha wafukue miili ya jamaa zao na ipelekwe katika makumbusho ya mauaji ya kimbari.
Familia yangu ilikataa lakini serikali ilitishia kuamrisha wafungwa waifukue miili hiyo, hatukuwa na la kufanya isipokuwa kwa jamaa zetu kufukua miili hiyo na kuipeleka katika makumbusho ya mauaji ya kimbari.

Bw Musonera aliongeza kwamba familia yake imesononeshwa sana na amri hiyo akisema walipoteza ndugu zao kwa njia ya kikatili.
Walistahili kupewa mazishi ya heshima, kilichotokea hakiaminiki, kwani alikuwa na uhusiano wa upendo wa hali ya juu kwa wazazi, ndugu, dada na marafiki waliopotea wakati wa mauaji, na kwamba hawezi tena kustahamili kuona mifupa yao ikining'inia maeneo ya makumbusho.
Hata hivyo chama cha manusura wa mauaji ya kimbari ambacho kina fungamano kubwa na serikali kinaunga mkono sera hiyo ya kufukua miili. Jean Pierre Dusingizemungu mkuu wa chama hicho anasema miili ya watu hao inapaswa kuwekwa katika maeneo hayo ili kuonyesha kilichotokea wakati wa mauaji.

Serikali ya Rwanda inataka miili ya kila muathiriwa wa mauaji ya kimbari yaonyeshwe hadharani ili kubainisha kiwango cha ukatili wa mauaji hayo.
Lakini wengi wanaoambiwa kufukua miili hiyo ya jamaa zao waliouwawa miaka 17 iliyopita, wangependelea wapumzike kwa amani mahali walikozikwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.