ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 27, 2011

CHAGUA MOJA KESHO :: KULIA AU KUCHEKA!!

Hayawi hayawi sasa yamekuwa! kile KiputeezZ cha Ukweli baina ya Mafahari wawili wenye mashabiki wengi' wengi' wengi' sana duniani na maadui wengi' wengi' wengi' duniani, Barcelona na Machester United kesho wanakutana uso kwa uso. Ingawa Manchester United inacheza katika ardhi ya Nyumbani (England), Barcelona kwa mujibu wa UEFA ndiyo watakuwa wenyeji wa mchezo huo kuikaribisha 'Man Yu'.

<--Messi katika dimba la Arsenal jana mara baada ya mazoezi.

Tayari Timu ya Barcelona imekwisha wasili nchini Uingereza kwaajili ya mpambano huo unao subiri masaa tu kuanza huku wakipewa hifadhi ya kutosha toka kwa Club ya Arsenal iliyotoa kiwanja chake kwaajili ya mazoezi ya wakali hao wanaohitaji kudhihirisha kuwa ndiyo wanaotisha dunia muzima kwa sasa.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 3:45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.


"KIFAA hiki tutakitumbukiza ndani ya kombe na kusepa" Ni kama wanazungumza vile Gerard Pique and Carles Puyol walipoiteua picha ya Fabregas katika ofisi za uwanja wa mazoezi wa Arsenal.

Ikumbukwe kuwa ni hawa hawa Pique na mwenzake Puyol ndiyo waliomlazimisha Fabregas kuvaa jezi ya Barca wakisherekea kombe la dunia mara baada ya kulitwaa pamoja kama timu ya taifa la Hispania.

Tayari kocha wa Machester United, Sir Alex Ferguson kasema kuwa atakitumia kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Schalke 04 kwenye nusu fainali ya michuano hiyo.


SWALI NI MAN U ama BARCA?
@g sengo

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.