Msichana Juliana akiwa nyumbani kwake akiandaa chakula kwa ajili ya wateja wake |
Na. Revocatus Herman
Tumeshuhudia jamii ikikumbwa na ukatili wa kijinsia hasa kwenye vipigo, lakini kwa msichana Juliana mambo yalikuwa ni tofauti yeye ni mtu aliyeonja ukatili wa kijinsia katika Nyanja ya kielimu. Baba mzazi wa Juliana aliamua makusudi kuelekeza ukatili wa kijinsia kielimu kwa binti yake, fuatilia makala hii yenye simanzi na masikitiko.
Baba hakutaka nisome kabisa, kwani kila mara nilipomwambia kuwa nahitaji kusoma aliniambia kuwa, kusoma kwa mtoto wa kike hakuna maana yoyote mtoto wa kike ana jukumu moja tu, ambalo nikuolewa. Alisema Juliana alipokuwa akinisimulia kisa chake huku akitokwa na machozi.
Juliana aliniambia kuwa kila mara alijitahidi kumshawishi Baba yake juu ya yeye kupelekwa shule lakini Baba yake alilirudia kauli yake kuwa, kusoma ni wajibu wa mtoto wa kiume. Baba yake Juliana alikuwa na watoto wane, watatu wakiwa wanaume, kwa upande wa watoto wa kiume wote walipelekwa shule kasoro ni Juliana tu ambaye alinyima haki ya kielemu.
Ni ukweli usiopingika kuwa kunyimwa kwa fursa kwa Juliana kulimfanya Juliana awepo hapo nilipomkuta, nilikutana na Juliana katika standi kuu ya mabasi ya Nyegezi Jijini Mwanza akiwa ameketi kwa hudhuni huku pembeni yake kukiwa na sufulia la uji wa ulezi aliokuwa akiuuza.
Kutokana na kuwa mapema sana asubuhi wateja walikuwa hawajafika eneo hilo, hivyo basi nilipata nafasi ya kumuuliza juu ya maisha yake yaliyomfanya ajikute kuwa mama lishe au ntilie , hapo ndipo aliporejea historia yake ya miaka kumi iliyopita iliyojaa uchungu na masikitiko ya ukatili wa kijinsia katika Nyanja ya elimu.
Juliana alisema kuwa kaka yangu namini leo hii na mimi ningekuwa kama mama Anne Makinda ambaye ni spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia, endapokuwa baba yangu hasingenitendea unyama wa kijinsia kwa kuninyima haki ya kuwa na elimu basi ningekuwa mbali kaka yangu, lakini ndiyo hivyo tena naishia kwenye kuuza uji.
Juliana aliniambia
kuwa, kaka yangu makubwa yalinipata kwani
nakumbuka mara kwa mara
nilikuwa namkumbusha baba
juu ya kiu
yangu ya kusoma, lakini kuna siku
sitaisahau, kwani nilipomkumbusha baba
juu ya suala hilo, aliishia kunipiga
huku akiniambia nishike
kichwa changu kwa mikono miwili
na kumzunguka alipokuwa amesimama
bila idadi ya mzunguko.
Ikumbukwe kuwa katiba
ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara
ya 13: 6 inasema ni marufuku kwa mtu
kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa
adhabu au kumdhalilisha.
Mimi naamini kama mwandishi natumia
nafasi hii kupinga
ukatili wa kijinsia hasa kwa kutumia mbinu
za za kuripoti ukatili
wa kijinsia kama TAMWA walivyoamua kuwajengea
uwezo waandishi wa habari kuripoti
matukio hayo.
Chama cha
wanahabari wanawake Tanzania
(TAMWA) kimekuwa kikipiga
kelele huu ya
ukatili wa kijinsia , lakini
bado kuna maeneo jamii inaendelea
na vitendo hivyo. Ni wazi
kuna Msichana Juliana
alinyimwa haki yake
ya kusoma kwa kuwa tu yeye
ni msichana, huo ni ukatili
mkubwa wa kijinsia.
Kwa sasa Juliana
anaendelea na biashara yake
ya mamaNtilie na
amejiwekea malengo ya
kukusanya fedha kidogo kidogo
na mwakani ana mpango wa kuanza kujiendeleaza
kielimu kwa kupitia elimu ya watu
wazima.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.