Mwanza
Baadhi ya watoto
yatima jijini Mwanza
wameangukia katika janga
la unyanyasaji wa kijinsia bila
jamii kujua vitendo
vinavyoendelea katika maeneo ya
watoto hao wa mitaani
hali maarufu kama (Ghetto).
Ilikuwa ni usiku wa saa
tano hivi nilifanikiwa kujichanganya
na kundi moja la watoto hao
wa mitaani, huku nami nikijifanya
ni muumini wa makundi hayo, nakumbuka ilikuwa ni
wa mtaa mmoja katika
barabra ya Nyerere,
kando ya barabara hizo
utakutana na nyumba za ghorofa, maeneo hayo
ndiyo makazi ya watoto hao wa mitaani pamoja na maeneo mengine jijini Mwanza.
Wakati nilipokuwa
katika kundi hilo la watoto wa
kike walishuhudia mwenzetu mmoja
akifanyiwa unyama mkubwa, kwani
lilitokea kundi jingine la wavulana watatu na kisha
kusogelea kundi hilo
na kuamua kumchukua binti
mmoja ambaye alikuwa amekaa
karibu na barabara na kisha kuingia
naye kwenye uchochoro
na baada ya muda
ilisikika sauti ya
binti yule ikiomba
msaada.
Licha ya
kelele zile zilizoashiria
kufanyiwa vitendo viovu vya kubakwa,
baadhi ya watu waliokuwa kipita eneo
lile waliendelea na
shughuli zao bila hata kuona
huruma kwa kwenda kutoa msaada. Nafikiri hali
hiyo inatokana na historia
ya vikundi hivyo
kuwa ni vya kinyama na
vinatembea na silaha mbalimbali vikiwemo
visu , nyembe na hata panga.
Bila shaka
unyama huo aliotendewa binti
huyo kwa mujibu wa Chama
cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), ukatili
huo unaangukia katika
kundi la ukatili wa saikolojia na
unaweza kusababisha mhusika kujinyonga.
Hapo ndipo nilipomuuliza mmoja wa marafiki wale
niliokuwa nao sehemu ile naye
akiwa ni mtoto wa mitaani, aliniambia
kuwa hali hiyo ni ya kawaida katika maisha yake ya mitaani na wao wameyazoea . Hapo ndipo nilipotaka kujua msaada
wowote wanaoupata hasa kutoka kwa askari wa doria, ndipo binti
huyo aliyejitambulisha kwa jina
Mary , ikiwa ni jina la bandia
nililompa aliniambia kuwa
hakuna msaada wowote
wanaoupata kwa askari wanaokuwa
doria, pindi wanapofanyiwa vitendo hivyo katili
Hapo nilizidi kupata picha nyingine tofauti
kwa kujiuliza inakuwaje hata mamlaka za usalama
kama jeshi la polisi kutotambua unyama huo wa watoto
wa mitaani ?. Kimsingi kunakuwa na makundi mengi ya watoto
hao wa mitaani, wanazidiana kwa rika na
umri, hivyo wale wakubwa wanakuwa
na sauti dhidi ya wale wadogo wanaoingia kwenye
maisha hayo.
Pia uchunguzi wangu ulibaini kuwepo kwa vyeo ndani
ya makundi hayo, kuna wanaojiita King, ikiwa ndiyo viongozi wa makundi, na kuna wale wa ngazi
ya kati wanaotumwa na viongozi
wao hasa kwenda kufanya
uhalifu sehemu fulani na kuleta watakachokipata huko.
Katika ukatili wa jinsia makundi
hayo yanahusika kwa kiasi kikubwa, kwani king
au mtawala anapohitaji
kufanya tendo la
ngono, basi atatoa amri ya kuletewa binti katika
maskani yake na wale
wa kati watatekeleza jukumu
hilo kwa kuhofia kupatwa
na adhabu kama watashindwa
kutekeleza jukumu hilo.
Ni muda muafaka
sasa jamii kusimama
na kuungana na Chama
cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania (TAMWA )kupinga ukatili
huo wanaofanyiana watoto
hao wa mitaani .
Nazo takwimu
za benki ya dunia zinaonyesha
kuwa wanawake wenye
umri wa kuanzia miaka
15 – 44 wapo katika
hatari kubwa ya
kubakwa kuliko kuugua saratani, kupata ajali , vita
na mlaria.
Pia licha
ya sheria ya
nchi inayoeleza kuwa endapo mtu
atabainika kuhusika kufanya ubakaji
atahukumiwa miaka thelathini
jela, lakini bado vitendo
hivyo vinaendelea, lakini swali la msingi ni nani
anasimamia vitendo hivyo kwa makundi kama watoto wa mitaani? Je watoto
hao wa mitaani wamepewa elimu
ya kuripoti vitendo
hivyo vya kinyama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.