Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) umewasilisha mpango kazi wa mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia Takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC) kupitia waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media).
Mpango kazi huo umewasilishwa leo Mei 20, 2019 jijini Dodoma kupitia kikao kazi kilichowajumuisha waandishi wa habari wa mitandaoni 23 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani.
Akiwasilisha mpango kazi huo, Victor Maleko ambaye ni Afisa Programu kutoka UTPC amesema pamoja na mambo mengine, umelenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mitandaoni kuzifahamu sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya Takwimu 2015, Sheria za Huduma za Vyombo vya Habari 2016 pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 ili kuripoti kwa weledi habari za utetezi na ushawishi wa haki za binadamu kwa kutumia takwimu.
Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Arusha (APC), Claude Gwandu amewataka washiriki wa mradi huo kuwajibika ipasavyo ili kuhakikisha unafikia malengo yaliyokusudiwa na kwamba klabu hiyo hakitakuwa tayari kuona mradi unakwama kutokana na baadhi ya washiriki kutowajibika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kundi la waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala kupitia mradi huo, Midraji Ibrahim amesema ili vyombo hivyo viendelee kuwa na manufaa katika jamii, lazima waandishi wake waweke habari zenye maudhui bora yakiwemo yanayogusa utetezi na ushawishi wa kutumia takwimu sahihi.
Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), unafadhiliwa na taasisi ya Freedom House ambapo ulianza mwaka jana 2018 ukitarajiwa kufikia tamati mwaka 2022.
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akifafanua jambo kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma.
Afisa Program kutoka UTPC, Victor Maleko akiwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia Takwimu (Data Driven Advocacy-DDA) kupitia kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Altenative Media).
Mwenyekiti wa Arusha Press Club (APC), Claude Gwandu akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Arusha Pres Club (APC), Claude Gwandu kwenye kikao kazi hicho.
Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema akifafanua jambo kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakimsikiliza Meneja Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania, Wakili Daniel Lema.
Mwenyekiti wa kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Alternative Media), Midraji Ibrahim (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wa kikao kazi hicho wakifuatilia mada.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho.
Washiriki wa kikao kazi hicho.
Kikao kazi hicho kimewajumuisha washiriki 23 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Washiriki wakifuatilia mada kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Washiriki wakifuatilia kikao kazi hicho.
Washiriki wakifuatilia mpango kazi wa utekelezaji Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa kutumia takwimu (Data Driven Advocacy-DDA), kupitia kundi namba tatu linalowajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbadala (Altenative Media) nchini Tanzania.
Washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika jijini Dodoma.
Walioshiriki kikao kazi hicho ni pamoja na Kadama
Malunde (Malunde Blog), William
Bundala (Kijukuu Blog), Merina
Makasi (Ngasa TV), Mohamed
Zengwa (Global TV), Eliya Mbonea (Mtanzania Digital), Midraji
Ibrahim (Sub Editor Mwananchi Digital), Mika Ndaba (Ayo TV), James Range (Sub Editor/ Programme Manager Global TV), Frankius
Cleophace (Cleo24 News and Dar Mpya), Asha Shabani (Asha Shabani TV), George
Binagi (Binagi Media Group), Albert G.
Sengo (GSengo Blog).
Wengine ni Francis
Godwin (Dar Mpya Blog/ Matukio Daima Blog), Abubakar
Kisandu (Kisandu Zenji Blog), Rashid Said
Rukungu (Rukungutz Blog CG Online Tv), Edither Karo (Correspondent (Michuzi Blog and Malunde Blog), Joseph
Mwaisango (Mbeya Yetu Online TV), Bakari
Chilumba (Correspondent Dar Mpya Blog, Millard Ayo, Mpekuzi na Muungwana), Abdulaziz
Ahmed (Lindi Yetu Blog na Lindi yetu Online TV), Gabriel
Kilamlya (Dar 24 Blog), Ibrahim Said
Limala (Correspondent Global TV online), Clavery
Christian (Muungwana Blog) pamoja na Hamza
Mashore (Ruvuma TV).
Maafisa Programu wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) nchini Tanzania wakiwa kwenye kikao kazi hicho.
Picha na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.