ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 20, 2019

MAFUNZO YA JINSIA KWA WANAHABARI KANDA YA ZIWA YAFIKIA TAMATI JIJINI MWANZA.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa (Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita) ili kuandika habari za kijinsia kwa weledi yamefikia tamati jijini Mwanza.

Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia jumamosi Mei 18, 2019 yaliandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na ile ya Vyombo vya Habari nchini Finland VIKES.

Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa alitumia fursa hiyo kuwahimiza waandishi wa habari Tanzania kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, misingi na miiko ya uandishi wa habari huku wakitoa usawa wa vyanzo vyao vya habari kwa kuzingatia jinsia.

"Bado vyanzo vingi vya habari vinawahusisha wanaume huku wanawake wakisahaulika hivyo mafunzo haya yawe chachu ya kuleta mabadiliko kwenye kazi zenu kwa kuibua na kutangaza masuala mbalimbali yanayowahusisha wanawake pia" alisema Gasirigwa.

Naye Maridhia Ngemela kutoka Radio Iqra FM ya jijini Mwanza aliyeshiriki kwenye mafunzo hayo alisema changamoto kubwa katika uandaaji wa habari na makala kwa kuzingatia jinsia ni baadhi ya wanawake kutokuwa tayari kutoa ushirikiano kama ilivyo kwa wanaume hivyo ni vyema elimu ikaendelea kutolewa ili kuondoa hali hiyo..

Hata hivyo mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Alex Mchomvu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza alisema suala la imani, mila na tamaduni mbalimbali linakwamisha usawa wa kijinsia hapa nchini hivyo waandishi wa habari ni vyema wakatumia nyenzo zao kutoa elimu ili kubadili fikra hizo na hivyo kuleta usawa wa kijinsia baina ya wanawake na wanaume.
Mkurugenzi wa MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa (wa tatu kulia) na Mkufunzi Kenneth Simbaya ambaye ni Mwenyekiti Mtandao wa Waandishi wa Habari za Afya Tanzania (wa pili kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzio hayo.
Mmoja wa wakufunzi, Alex Mchomvu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza akiwasilisha mada kwenye mafunzi hayo.
Washiriki waki-refesh viungo vya miili yao kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakimsikiliza Mkufunzi, Kenneth Simbaya wakati akiwasilisha mada.
Mkufunzi, Kenneth Simbaya akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washirikiwa wakiwa kwenye majadiliano kupitia makundi.
Mwanahabari mkongwe, Florah Magabe (kushoto) pamoja na mwanahabari chipukizi, Sefroza Joseph (kulia) wote kutoka jijini Mwanza, wakifurahia jambo kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia jambo kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa umakini jambo kwenye mafunzo hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.