Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amewasili katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo, kwa ajili ya kuhudhuria kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge akiwa ameongozana na Mbunge wa Ileje (CCM), Janeth Mbene.
Spika wa Bunge, Job Ndugai aliagiza kabla ya saa 5 leo asubuhi, Mbunge huyo awe amewasili bungeni kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kujibu tuhuma zinazomkabili za utovu wa nidhamu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.