Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Simon Sirro amesema kuwa, maeneo ya viwanja vya ndege hususani kiwanja cha ndege Dar es salaam kamwe hakitakuwa uchochoro wa kupitisha na kusafirisha magendo, biashara ya binadamu, nyara za serikali pamoja na dawa za kulevya.
IGP Sirro ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal III kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanja hicho ambacho hadi sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.