Theresa May kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Conservative tarehe 7 Juni na kutoa fursa kuidhinishwa mchakato wa kuchaguliwa waziri mkuu mpya Uingereza.
Katika taarifa iliojaa hisia alioitoa huko Downing Street, Bi May amesema amefanya "kila awezalo" kutekeleza matokeo ya kura ya maoni kuhusu EU ya mnamo 2016.
Ni jambo linalosalia kuwa "na majuto mengi" kwamba ameshindwa kutimiza Brexit - Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, ameongeza.
Lakini waziri mkuu mpya ndio suluhu " kwa manufaa ya taifa".
Bi May amesema ataendelea kuhudumu kama waziri mkuu wakati kukitarajiwa kuidhinishwa mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa chama cha Conservative.
Atajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Juni 7 na uteuzi wa waziri mkuu mpya unatarajiwa kuanza wiki inayoafuata baada ya hatua hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.