ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 22, 2019

GAVANA AAGIZA UTENDAJI MZURI MAKAZINI.

picha ikionyesha Mkurugenzi Mkuu wa Bodi yaTaifa ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu(NBAA),Pius Maneno akoongea na waandishi wa habari hii leo

picha ikionyesha baadhi ya washiriki pamoja na viongozi wakiwa katika picha ya pamoja

Na Woinde Shizza,Arusha
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT)Florence Luoga,amewaagiza wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya kazi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi zao kwa weledi ili kuepuka malalamiko ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakiikumba kada hiyo
Aliyasema hayo leo alipokuwa akifungua mkutano wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini(NBAA)unaondelea jijini hapa na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutaongeza imani ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu kwa jamii na taasisi wanazozihudumia.
“Ni vyema wahasibu kote nchini kuhakikisha kuwa malipo yote yanayofanyika yapitie katika taasisi za kifedha,ikiwemo mabenki taasisi hizo ziweze kujiendesha na serikali iweze kujiongezea kipato kwa lengo la kukuza pato la Taifa”alisema Luoga.
Ameongeza kuwa endapo watafuata utaratibu huo utasaidia kuondokana na changamoto ya malipo hewa pamoja na kukabiliana na tatizo kubwa la uingizwaji na uzagaaji wa fedha haramu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi yaTaifa ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu(NBAA),Pius Maneno amesema kuwa lengo la mkutano huo wa siku tatu ni kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu.
Ameongeza kuwa katika mkutano huo mada kumi na moja  zitawasilishwa na kujadiliwa zikiwemo za fedha,Tehama,uadilifu pamoja na muongozo wa wahasibu na wakaguzi wa mahesabu kuhusiana na suala zima la fedha haramu ikiwemo kanuni za nidhamu.
“Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini imeendelea kuwaelimisha wahasibu na wakaguzi wa mahesabu hapa nchini juu ya kufanya kuzingatia wajibu na weledi pindi watekelezapo majukumumu yao ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wale wote wanaokiuka maadili”alisema Mkurugenzi mtendaji huyo.
Mkurugenzi mtendaji huyo amesema kuwa bodi yake imetunga muongozo ulioanza kutumika tarehe 1aprili  mwaka huu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kuhakikisha kuwa wanakagua mahesabu yao lengo likiwa ni kuongeza kodi na tarehe 1 mei umeanza kutumika  muongozo wafedha hamu na tarehe 15juni zitaanzakutumika kanuni za uadilifu.
Amesema kuwa mkutano huu unashirikisha watu mia tatu ambao ni wahasibu na wakaguzi wa hesabu z kutoka taasisi na mashirika mbalimbali,maafisa kutoka Benki Kuu(BOT),nabenki nyinginezo,wataalamu wa fedha na taasisi za Bima.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.