MNYAMA Simba ameelezwa ndiye
anayevutia idadi kubwa ya watalii wanaoitembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha
inayotajwa kuwa na kiwango kikubwa cha wanyama hao nchini na kwa bara zima la
Afrika.
Wakizungumza wakati wa ziara ya
Utalii ya maafisa Tarafa na Watendaji kutoka wilaya ya Iringa iliyoratibiwa na mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo, walisema kuwa wamefurahishwa na namna hifadhi
hiyo ilivyokuwa na vivutio vingi ambavyo vipo ndani ya hifadhi hiyo kama
vile mnyama Simba.
Stella makali na Aunt Mbilinyi ni
watendaji wa kata walisema kuwa wamefurahi kufanya utalii katika hifadhi ya
Taifa ya Ruaha baada ya kuona namna ambavyo mnyama Simba anavyofanya mapenzi
jambo ambalo
hawajawahi kuliona toka wanzaliwe hivyo inawafanya watafute muda mwingine wa kwenda
kufanya utalii katika hifadhi hiyo.
Walisema kuwa wamefurahia kutembelea
hifadhi hiyo kwa namna ambavyo wameona wanyama Simba anavutia kiasi kwamba ukiwa
katika hifadhi hiyo utakuwa na furaha muda wote kwa namna ambavyo vivutio
vingi vilivyopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
“Tumerithishwa,Tuwarithishe tuungane
kwa pamoja kuokomeza ujangili katika hifadhi yetu ya Ruaha iliyopo mkoa wa Iringa
ili hata watoe watu waje waone wanyama na vivutio vilivyomo hifadhini”alisema
makali
Emmanuel Ngabuji ni kaimu Afisa
Tarafa Pawaga alisema kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha imejaliwa kuwa na vivutio
vingi ambavyo mtalii akifika katika hifadhi hiyo atafurahia na hatatamani
kuongoka kutoka kuwapata furaha awepo kwenye hifadhi hiyo ikiwa na kumuona
mnayama Simba ambaye amekuwa kivutio kikubwa.
Ngabuji alisema kuwa watendaji wengi
imekuwa mara yao ya kwanza kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kumshuhudia
mnyama Simba akiwa katika fungate jambo ambalo liliwafurahisha watalii wote
walikuwepo katika hifadhi hiyo ya taifa.
“Simba
ni mnyama anayependwa katika historia yake yote, na ni ishara ya ujasiri na
nguvu. Wanyama hawa kitabia wana miili yenye nguvu—na miungurumo inayoweza
kusikika kutoka umbali wa maili tano,” alisema.
Ngabuji alisema kuwa wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akiutangaza
utalii wa ndani kupitia filamu ya Royal Tour ambayo imeanza kuleta matokeo
chanya ya ongezeko la watalii nchi na watalii wa ndani kuongezeka kutembelea
vivutio mbalimbali.
Naye Menaja Msaidizi wa Hoteli ya
Jabali Asili, Josina Mkundi alisema; “Filamu ya Royal tuwa imewaongezea wageni
wengi wa kimataifa wanaotembelea hifadhi hiyo na kujionea vivutio vyake lukuki,
akiwemo mnyama Simba. Navyoongea sasa hoteli yetu imejaa.”
“Tuna wageni
wengi kutoka Uingereza, Ujerumani na Marekani. Pamoja na kufurahia manzari
nzuri ya hifadhi hii, wanyama wakubwa na wadogo na aina mbalimbali za ndege,
mnyama wanayetaka kumuona zaidi na bila kuchoka ni Simba.”
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa lengo la kuwapeleka maafisa Tarafa na watendaji kutalii katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni kutambua umuhimu wa utalii na namna ambavyo wanaweza kuwalinda wanyama pori wasitoweke ili kuwaliaisha wananchi wengine.
Moyo alisema kuwa maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha kunaongeza chachu ya ongezeko la watalii katika ukanda wa nyanda za juu kusini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kusisimua uchumi kupitia sekta hiyo muhimu nchini.
Alisema kuwa mnyama Simba amekuwa kivutio kikubwa kwa watalii ndio maana mtalii asipoona Simba anahisi kama hajafanya utalii, “leo maafisa Tarafa na watendaji wamefanikiwa kumuona Mnyama Simba akiwa fungate jambo ambali limefurahisha sana”.
Mohamed
Moyo alisema barabara hiyo itajengwa kupitia sehemu ya mkopo wa masharti
nafuu wa Sh Trilioni 1.2 uliotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya
kuboresha usalama, ustahimilivu wa tabianchi, uwezo wa barabara za ndani na
viwanja vya ndege vya mikoa.
Mmoja wa watalii hao kutoka
Ujerumani, Romy Wagner alisema mbali na kushuhudia kwa macho yake aina
mbalimbali za wanyama na uoto wa asili hifadhini humo, shauku yao ilikuwa
kuwaona Simba kwa macho yaolakini pia waliona chui saba wakiwa katika kundi
moja, juu ya mti.
Naye dereva wa mkuu wa wilaya ya Iringa
Ramadhan Sosovele alisema makundi makubwa ya nyati, tembo na simba yalikua
kivutio chao kikubwa na akafichua kwamba watendaji na maafisa tarafa wengi wao
ni mara yao ya kwanza kuwaona wanyama hao katika maisha yao ya asili hifadhini
tofauti na walivyozoea kuwaangalia katika filamu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.