Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino hatimaye amekubali kwamba kinara wa chama chake Raila Odinga alishindwa katika uchaguzi wa Agosti 9 dhidi ya Rais William Ruto. Babu Owino alisema hatimaye alikubali kwamba Raila alishindwa katika uchaguzi wa Agosti 9.
Babu anaonekana kukubali matokeo ya uchaguzi huo baada ya kiongozi wa nchi kuhutubia kikao cha pamoja cha bunge mapema Alhamisi, Septemba 29.
Akitumia majukwaa yake ya mitandaoni, mbunge huyo mchanga alibainisha kuwa amekiri Raila alipoteze na kuongeza kuwa yuko tayari kuwa katika upinzani. “Leo nimeamini hii kitu ilienda kweli. Ni kama Ndoto.
Sasa, lazima tupate wadhifa wa mwenyekiti wa PAC na pia tuipige serikali darubini," alisema.
Haya yanajiri siku chache baada ya Babu kuonya chama cha Orange Democratic Movement dhidi ya mipango ya kumteua mbunge John Mbadi kuchukua wadhifa wa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu.
Mbunge huyo mwenye utata aliapa kutomwachia Mbadi, ambaye alikosa nafasi ya kiongozi wa wengi bungeni. "Chama cha ODM, kwa heshima inayostahili, kwa nini John Mbadi ashuke kutoka wadhifa wa kiongozi wa Wengi hadi uenyekiti wa PAC, ambao nilitengewa mimi?
Hili halitafanyika!!! Sitakubali," Babu alisema kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Babu alisema umefika wakati kwa wabunge vijana kuchukua nafasi za uongozi, akisisitiza kuwa tayari chama kimemzawadia Mbadi na nafasi ya kuteuliwa katika Bunge la Kitaifa.
Kwa upande wake, Mbadi alipuuzilia mbali madai ya Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kwamba ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Uhasibu ya Umma (PAC).
Katika Hotuba Yake ya Kwanza Bungeni Wakati wa mahojiano na NTV mnamo Ijumaa, Septemba 23, Mbadi alisema chama hicho hakina mamlaka ya kuchagua wenyekiti wa kamati.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.