ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 23, 2017

DC GONDWE AWATAKA WANANCHI WASICHOKE KUCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA AFYA

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiongea na wananchi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kushirikiana na nguvu za wananchi, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitokea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua kimaendeleo. PICHA NA KAJUNASON/MMG - HANDENI, TANGA.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akimsaidia Diwani wa Kata ya Kwamgwe, Sharifa Abebe alipokuwa akitoa machozi ya shukrani kwa shirika la maendeleo la World Vision Tanzania kwa kuweza kushirikiana na wananchi kuwajengea jengo la zahanati lililoweza kugharimu shilingi milioni 190 ambapo wao World Vision Tanzania waliweza kutoa Milioni 100 na wao wananchi waliweza kujitoa kwa nguvu zao kwa thamani ya milioni 90. Hafla hiyo ilifanyika katika Kata ya Kwamgwe ambapo ndipo jengo hilo lilipojegwa.
Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania,  Humphrey Bernard akisoma risala ya mradi wa ujenzi wa zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwamgwe ambapo aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha ujenzi wa jengo la zahanati.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akikabidhiwa mikataba wa zahanati na mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP wa World Vision Tanzania, Humphrey Bernard (kushoto) ambao ndiyo waliojenga kwa kushirikiana na wananchi waliojitoa kwa hali na mali.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Handeni, William Makufwe akitoa ufafanuzi jinsi wananchi walivyoweza kujitoa ujenzi wa zahanati.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Dokta Credianus akitoa nasaha zake kwa wananchi wa Handeni waweze kujua umuhimu wa kuwekeza katika afya. Jengo la zahanati iliyojengwa katika Kata ya Kwangwe, Wilayani Handeni.
Wakati huo huo, mkuu wa wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akipokea zawadi ya kuku kutoka wa mwenyekiti wa kitongoji cha Migombani, Michungwani-Segera Bi. Amina Njama ambaye amekuwa msitari wa mbele katika uhamasishaji wa kukusanya matofali ili yaweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa na zahanati.
 Mkuu wa Wilaya akifurahi na viongozi.
 Mkuu wilaya akipata maelezo machache kutoka kwa wananchi waliitikia wito wa kuchangia maendeleo kwa kuchimba msingi wa zahanati ya  Migombani, Michungwani - Segera.
Mkuu wa Wilaya akiwashukuru wananchi kwa moyo wao wa kujitolea katika maendeleo. Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewataka wananchi wa Kata ya Kwamgwe kuendelea kujitoa kikamilifu katika kuchangia shughuli za kijamii ili kuendana na kasi ya rais Dkt. John Magufuli katika kuleta maendeleo endelevu. 

Akizungumza na wakazi wa Kata ya Kwamgwe wakati akikabidhiwa zahanati iliyojengwa kwa hisani ya shirika la maendeleo la World Vision Tanzania, mkuu wa wilaya aliwaomba wananchi waendelee na moyo wa kujitolea katika kuchangia kazi za maendeleo ili kijiji kiweze kujikwamua. "Nawaomba ndugu zangu, sisi wote ni wanaKwamngwe, lazima tuamue kuchangua mambo muhimu matatu, kutambaa, kutembea au kukimbia. 

Jambo la msingi ni lazima tuwe katika mwendo, tuendelee kujitoa tuzidi kuleta maendeleo kijijini kwetu," alisema Gondwe. Awali akikabidhi mradi huo wa zahanati hiyo, Mwezeshaji wa mradi Mkumburu ADP, Humphrey Bernard aliwashukuru wananchi wa kata ya Kwamgwe kwa kuweza kujitoa kufanikisha ujenzi wa jengo la zahanati. 

Wakati huo huo, Mkuu wa wilaya Handeni aliweza kutembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Michungwani, Segera ambapo ujenzi wake unaanza hivi karibuni kwa nguvu za wananchi kupitia kampeni ya mkuu huyo ya kuongeza zahanati na madarasa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.