ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 23, 2017

HAPA NDIPO LULU ANAPO LALA GEREZANISiku ya pili leo inakatika wakati ambapo mwigizaji nyota wa filamu nchini Tanzania Elizabeth Michael 'Lulu' akiwa nyuma ya nondo za gereza la Segerea jijini Dar es salaam, hii ikiwa ni mara baada ya maamuzi wa Mahakama dhidi yake yakimuamuru kutumikia kifungo cha miaka miwili baada ya kukutwa na kosa la kumuua bila kukusudia, aliyekuwa Nguli wa Filamu nchini Steven Kanumba 'The Greatest' Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku,mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi. 

Moja ya maswali kati ya mengi yaliyotawala vichwa vya wengi:- 
 1. Maafisa magereza walimpokeaje Lulu huko gerezani? 
2. Jeh ni kweli kuwa watu maarufu wanapokuwa kifungoni huwa na maeneo yao spesheli yenye full service, Jeh msanii huyo baada ya kutupwa Segerea analala wapi? 
3. Mfungwa anapohukumiwa miaka yake kadhaa, Jeh hesabu ya miaka hiyo huwa kwa mtindo upi? ---Jeh Usiku na Mchana huhesabika kama siku mbili au imekaaje?
4. Jeh Lulu ana qualify kupata msamaha wa Rais? 

KAZI NA NGOMA ya Jembe Fm chini ya Mwenyekiti Albert G. Sengo naye Katibu Mansour Jumanne inamtafuta Afisa wa jeshi la Magereza ambaye ni Msemaji wa Jeshi hilo Lucas Mboje na kufanya naye mahojiano.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.