Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akifuatilia kwa karibu maendeleo ya wanafunzi wa kidato cha Tatu shule ya Sekondari Kakubilo Halmashauri ya Geita baada ya kutembelea shule hiyo na kutoa swali la Hisabati kwa wanafunzi hao.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita akikabidhi fedha shilingi 2,400,000/= kwa Diwani wa Kata ya Ludete Sebastian Mranda kwa ajili ya ujenzi wa boma la Zahanati ya Kijiji na Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika hiyo.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akishirikiana na wananchi wa Kata ya Ludete Wilayani Geita kumwaga zege kwa ajili ya lenta kwenye ujenzi wa madarasa 10 ya shule ya msingi Ludete yenye wanafunzi 6,616 alipokwenda kuzindua kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Wananchi wa kijiji cha Ludete Kata ya Ludete Wilayani Geita wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kijiji hicho kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Geita za kila kijiji kuwa na Zahanati.
Wananchi wa kijiji cha Ludete Kata ya Ludete Wilayani Geita wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kijiji hicho kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Geita za kila kijiji kuwa na Zahanati.
WANANCHI KATA ZA LUDETE, KAKUBILO
WAMKOSHA RC GEITA UJENZI WA ZAHANATI NA MADARASA ACHANGIA TOFALI 2000,MIFUKO 420 YA SARUJI
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za ujenzi wa
Zahanati na Shule kata za Ludete na Kakubilo Halmashauri ya Geita kwa kuchangia
matofali yenye thamani ya shilingi 2,400,000/= na kufanikisha harambee ya
mifuko ya Saruji zaidi ya 420.
Mhandisi
Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za wananchi baada ya kutembelea kata hizo na kuridhishwa
na kazi za ujenzi wa Zahanati za vijiji na Shule zinazofanywa na wananchi kwa
kujitolea kufanya kazi bila malipo, kuchangia vifaa mbalimbali vya ujenzi na
kuchimba misingi.
Akiwa
Kata ya Ludete Mkuu wa Mkoa amesema " Nimefurahi sana kuona namna
mnavyoshiriki katika utekelezaji wa miradi hii niwaombe mshiriki kuanzia mwanzo
hadi mwisho na msikubali mtu yeyote kuwavunja moyo kwa kuwa maendeleo ya Ludete
yataletwa na wananchi wenyewe hivyo mimi ninawachangia matofali 1000 kwa ajili
ya Zahanati na mengine 1000 ya kujenga vyumba vya madarasa shule ya Sekondari
Ludete".
Awali
akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Diwani wa Kata ya Ludete Sebastian Benedicto Mranda
amesema kuwa wananchi wameamua kujitolea kushiriki ujenzi wa Shule mpya ya msingi baada ya shule
ya Msingi Ludete kuwa na Idadi ya wanafunzi 6,616 huku kukiwa na madarasa 20 yenye mikondo 108
ambao unasababisha msongamano wa wanafunzi darasani.
Marando ameongeza kusema
kuwa Kata ya Ludete haina Zahanati kwa muda mrefu hivyo wananchi
wamejihamasisha kujenga ili wapate huduma katika maeneo yaliyo jirani pia
kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kuhakikisha kila
kijiji kinakuwa na Zahanati na shule ya msingi na Sekondari kwa Kata, Kata ya
ludete ina wanafunzi 900 wanaotarajia kujiunga na elimu ya Sekondari ikiwa na
uhaba wa zaidi ya vyumba vya madarasa 20.
Katika
ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa amefanya harambee ambayo imefanikisha upatikanaji wa
mifuko ya Saruji zaidi ya 420 na kuziagiza Halmashauri kutumia vikundi vya
mafundi waliokatika maeneo ya miradi ili kupunguza gharama na kusimamia
matumizi ya fedha za miradi hiyo.
Kutokana
na Mkoa wa Geita kuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati Serikali imeamua
kushirikiana na wananchi kufanya kampeni ya mkoa mzima kuhamasisha wananchi
kujitokeza kushiriki na kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo ili wananchi
wapate huduma katika majengo bora na mazingira salama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.