Baadhi ya raia kutoka Jamuri ya Kidemokrasia ya Congo DCR wakifuatilia ujio wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma ilipowasili kukagua kituo cha Kigadye Wilayani Kasulu.
Baadhi ya raia kutoka Jamuri ya Kidemokrasia ya Congo DCR wakifuatilia ujio wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma ilipowasili kukagua kituo cha Kigadye Wilayani Kasulu.
Mmoja wa waomba hifadhi akieleza mbele ya Kamati ya Ulinzi ya Mkoa sababu zilizo wafanya wakimbilie Tanzania
Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR Kigoma(mwenye kofia ya bluu) akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma hali ya kituo cha kupokelea Wakimbizi Kigadye.
ZAIDI YA RAIA 800 KUTO CONGO WAKIMBILIA KIGOMA KUHOFIA AMANI
Takribani raia 800 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wamekimbilia
Nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi katika kijiji cha Kigadye Wilayani
Kasulu, Mkoani Kigoma wakihofia machafuko.
Raia hao ambao wengi wao wanatoka maeneo ya Fizi na misisi Kivu kusini mwa
Congo wamedai kuwa Vikosi na wapiganaji wa maimai nchi Congo na vikundi
mbalimbali vya waasi vinavyoendelea kupigana nchini vimewatia hofu na hivyo
kuanza kukimbia nchini Tanzania kuomba hifadhi ya ukimbizi.
Wakizungumza mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma
iliyotembelea katika kituo cha kupokelea waomba hifadhi kijiji cha Kigadye raia
hao walisema sababu iliyowafanya kukimbilia Tanzania ni hofu ya usalama wa
maisha yao kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya vikundi vya waasi na
Serikali iliyopo madarakani.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (mst.) Emannuel Maganga
akiongoza kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa amesema tayari Mkoa umefika
kuwaona raia hao na wanafana jitihada za kuhakikishah wanapatiwa huduma
muimu za kibinadamu zinaboresha katika eneo hilo wakati kamati ya taifa ya
kusikiliza maombi ya ukimbizi inajiadaa kuwasikiiza raia hao.
Kutokakana na wimbi kubwa hilo huduma za kibinadamu ikiwemo chakula, malazi
zinahitajika haraka ili kuwahudumia raia hao ambao wengi wao ni kinamama na
watoto.
Baadhi ya raia waliokimbilia nchini Tanzaia wamedai kuwa kutokana na
kuahirishwa Uchaguzi Mkuu uliopaswa kufanika Desemba, 2017 dalili za kuzuka
kwa mzozo wa mapigano uenda ukawaathiri amani nchini Congowa, Vyama vya
upinzanu vimeanza kuonesha dalili za kupinga kusitishwa kwa uchaguzi,
wamehofia amani.
Kituo cha kigadye wilayani kasulu, huenda kikashindwa kimili idadi kubwa ya raia
wa Congo wanaoendelea kfika kituoni hapo kwa madai ya kukimbia vita nchini
mwao. Kusini mwa Congo kumekuwa na matukio ya hivi karibuni mashambulio
ya mara kwa mara yanayosabisha hofu ya machafuko kwa wananchi.
Habari na Picha zimeandaliwa na.
Gabriel Ng’honoli
Afisa Habari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.