
Televisheni inayomuunga mkono Kanali Gaddafi, al-Urubah, imesema Kanali Gaddafi ambaye bado hajulikani alipo, ametoa hotuba akisema kuondoka kutoka kwa makazi yake kulikuwa ni ''mpango''.
Makazi hayo ndiyo yaliyokuwa maeneo ya mwisho chini ya udhibiti wa Kanali Gaddafi mjini Tripoli. Waasi wamekuwa wakisheherekea mafanikio yao katika bustani ya Green Square, mjini Tripoli.

Hata hivyo bado mapambano yanaripotiwa katika mji huo, mkiwemo katika maeneo ya Abu Salim na Hadba na karibu na hoteli ya Rixos, ambapo waandishi wa kigeni wanapoishi.
Mwandishi wa BBC Rana Jawad mjini Tripoli amesema kuwa kuna hisia kuwa huu ndio mwisho wa utawala wa Kanali Gaddafi, lakini sherehe kamili hajitaanza hadi pale yeye na jamaa wake watakapo kamatwa.

Kanali Gaddafi aidha amesema makazi yake yameharibiwa na mashambulio 64 ya angalini ya NATO. Jumanne asubuhi, wapiganaji wa waasi waliokuwa wamejihami vilivyo walimiminika katika mji mkuu kushiriki katika mashambulio ya Bab al-Aziziya.


''Tumeshinda makabiliano'' Abdul Hakim Belhaj, kamanda wa ngazi ya juu wa waasi mjini Tripoli aliliambia shirika la al-Jazeera.''Wametoroka kama panya''.
Haijulikani iwapo kanali Gaddafi na jamaa wake walikuwa katika makazi hayo ya Bab al-Aziziya, lakini inaripotiwa kuwa ina mahandaki ya chini kwa chini, yanayounganisha na maeneo mengine ya mji.
Hali sio wazi katika katika mji wa Sirte, alikozaliwa Kanali Gaddafi, ambayo imekuwa ngome ya maafisa wanaomuunga mkono. Ripoti zinasema wanajeshi waliorudishwa nyuma wanaelekea huko.
Tupe maoni yako
Sasa imekua maneno tu kwa Gaddafi hana lake tena na mwisho wake utakua kama Saddam ni kula kamba.
ReplyDeleteHuyu jamaa si wa kumuua ni wa kumkausha halafu anawekwa katika maonyesho Libya watatajirika zaidi kwa kupata watalii toka pande zote za dunia kumuona huyu jamaa, Au awekwe awe mchekeshaji aktika mikutano ya taifa na tv.
ReplyDelete